Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Halima James Mdee

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HALIMA J. MDEE aliuliza: - Je, ni lini Serikali italipa madai ya shilingi trilioni 7.91 ya watoa huduma kama yalivyoripotiwa kwenye ripoti ya CAG 2021?

Supplementary Question 1

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa madeni haya shilingi trilioni 7.9 kama ulivyosema ni ya wafanyakazi, watoa huduma na wauzaji bidhaa na ni ya muda mrefu, hauoni kwamba Serikali mnakuwa sehemu ya kufifisha shughuli za kiuchumi za Watanzania? Swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili; Wizara yako ya Fedha ndio inayomsimamia Msajili wa Hazina, sasa ni lini mkakati huu utakamilika, nataka time frame ili mkakati huu upelekwe kwenye Kamati ya Bunge inayosimamia mashirika ya umma kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji? Ni lini? Time frame? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima James Mdee, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mipango ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tumelipa madeni yote hasa Serikali ya Awamu ya Sita, tumelipa madeni yote yaliyopo katika Serikali, lakini ni lini mkakati huu utaanza kutumika ni wakati wowote baada ya kupitia na kuhakiki wataalam wetu basi itatolewa taarifa rasmi. Ahsante. (Makofi)