Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kuvuna maji katika Mji wa Itigi?

Supplementary Question 1

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Swali langu nimeulizia Mji wa Itigi ila imejibiwa vijijini. Basi, sasa je, Serikali ipo tayari sasa kuvuna maji katika Mji wa Itigi ili kujenga bwawa linaoitwa Mkalamani ambalo lipo palepale Mjini Itigi?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kujibu swali lake la nyongeza la kuvuna maji katika Mji wa Itigi.

Mheshimiwa Spika, Mji wa Itigi ni moja ya Miji ambayo upatikanaji wake wa maji unaendelea vizuri kwa sasa ni zaidi ya asilimia 70. Kwa hiyo, kwenye masuala ya uvunaji wa maji tunazingatia zaidi maeneo ambayo maji yanapatikana kwa shida zaidi, lakini pale itakapobidi basi tutafanya hivyo.