Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya TFS/TANAPA na wananchi wa Kata za Inyala, Itewe na Ilungu?

Supplementary Question 1

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Inaelekea kuna mkanganyiko kidogo kwenye majibu ya Serikali, kwa sababu mwaka 2007 wananchi wa Kata ya Ilungu hususan Kijiji cha Kikondo walifanyiwa tathmini ya kupewa fidia kwa yale maeneo yaliyochukuliwa na DAFCO ambayo sasa hivi ndiyo Hifadhi ya Taifa ya Kitulo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hali hiyo wenzetu wa TANAPA walishindwa kuwafidia wale wananchi, kwa hiyo yale maeneo hasa Kijiji cha Kikondo bado yanatumika ni kijiji ambacho kina shule kina zahanati. Pia kuna maeneo ambayo yalichukuliwa na watu wa TFS kwenye Misitu ya Mwambalis na hayo maeneo yamekuwa yakitumiwa na wananchi hata kabla ya hapo na mpaka leo yanatumiwa.

Sasa kutokana na mkanganyiko wa majibu, naomba Mheshimiwa Waziri apange ziara akayatembelee hayo maeneo ili afanye tathmini yeye mwenyewe ili kujua uhalisia, lakini hali siyo nzuri kuna mgogoro na wananchi kwa kweli wanapata shida sana. Nashukuru. (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oran Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto hizi ambazo mara nyingi wananchi wamekuwa wakihitaji ardhi wakati huo huo maeneo haya yalichukuliwa na Serikali. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto hizi tutaenda kuzifuatilia, lakini pia tutaenda kukutana na wananchi ambao wamekutana na kadhia hii na lengo ni kukaa pamoja ili kuweza kutatua changamoto hii. Hivyo nitafika kwake kwenda kutatua changamoto hii. Ahsante.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya TFS/TANAPA na wananchi wa Kata za Inyala, Itewe na Ilungu?

Supplementary Question 2

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante hili suala la Hifadhi ya Kitulo liko pia Makete ambako ni wilayani kwangu. Kuna mgogoro mkubwa kati ya wananchi na Hifadhi ya Kitulo kwa sababu uwekaji wa beacon ya mipaka haukushirikisha wananchi kitu ambacho kimesababisha mgogoro mkubwa. Pia tuna hifadhi ya Mpanga Kipengele ambako kuna Vijiji vya Ikovo, Kimani na kwenye Hifadhi ya Kitulo mgogoro mkubwa uko kwenye Vijiji vya Chankondo, Misiwa kule Itelele.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Bunge hili ilituahidi kwamba itakuja Makete kutatua hii kero na haijaja hadi leo. Ile timu ya Mawaziri Nane pia ilisema itafika Makete haijafika hadi leo.

Je, ni lini Serikali itakuja kutatua changamoto hii ya migogoro ili wananchi wangu waweze kupata maeneo kwa kufanya kazi kwa sababu ndiyo waliotumia kuhifadhi hii Hifadhi ya Kitulo hadi Serikali imekuja kuichukua mwaka 2005?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, Mbunge wa Makete, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na maelekezo ya Mheshimiwa Rais ambaye aliandaa Kamati ya Mawaziri Nane ambao walikuwa wanapaswa kuzunguka nchi nzima. Zoezi hili tulilianza kipindi cha mwaka uliopita na tulizunguka kwenye baadhi ya maeneo. Nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Sanga kwamba zoezi hili bado ni endelevu tutafika kwenye maeneo yote yenye migogoro na tutatatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, yale ambayo yameshapitiwa na kamati hii tutahakikisha kwamba yanarudishwa kwa wananchi. Yale ambayo ni migogoro mipya Mheshimiwa Waziri ameshaunda kamati nyingine ambayo tumeanza kupitia tena upya maeneo ambayo yana migogoro ili kuhakikisha kwamba wananchi na maeneo ya hifadhi yanahifadhiwa vizuri na wakati huo huo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku. Ahsante.

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya TFS/TANAPA na wananchi wa Kata za Inyala, Itewe na Ilungu?

Supplementary Question 3

MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kama kuna mkoa ambao ulikuwa unasubiri kwa hamu ile Timu ya Mawaziri Nane ni mkoa wa Morogoro. Jimbo la Mikumi, Kata za Zombo, Muhenda, Kisanga na Mikumi zimekuwa katika changamoto ya muda mrefu ya mipaka kati yao na TFS, kati yao na TANAPA.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba kuna timu ambayo imeundwa na Waziri kuorodhesha migogoro hiyo. Je, kata hizo na vijiji hivyo vya kata hizo zinaenda kuingia katika orodha ndefu ya vijiji vyenye migogoro? Nawakilisha.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili naomba nilifafanue kwa ufasaha zaidi kuna ile migogoro ambayo inapitiwa na Mawaziri Nane. Hii migogoro Mawaziri Nane watapita kwenye maeneo nchi nzima na watatatua hii migogoro. Hata hivyo, kuna migogoro mipya ambayo haikuwahi kupitiwa na Kamati ya Mawaziri Nane. Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ameunda Kamati ndani ya Wizara imehusisha na maeneo mengine kwa maana ya watumishi wa ardhi na maeneo ya mazingira kupitia mapori ya hifadhi, kupitia ramani moja baada ya nyingine kuangalia huu mgogoro unatoka wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna migogoro mingine ni ya beacon, kuna migogoro mingine wamesogea kidogo, kwa hiyo kuna mabishano kati ya mipaka na mipaka. Kamati hii itapita tena upya na itaangalia pale ambapo pana mgogoro tutautatua kwa pamoja na tutazisoma ramani tuta- define mipaka na baadaye tutatoa majibu sahihi ili wananchi waridhike na maeneo ya hifadhi, lakini wakati huo huo watendewe haki kuliko ilivyo sasa. Ahsante.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya TFS/TANAPA na wananchi wa Kata za Inyala, Itewe na Ilungu?

Supplementary Question 4

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwanza nianze kuipongeza Wizara ya Maliasili kwa kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Nyangh’wale kuweza kutokomeza wanyama wakali kama vile fisi ambao walipoteza maisha ya wananchi wangu wa Jimbo la Nyangh’wale. Sasa swali, je, ni lini Waziri atapanga ziara ya kuja kuwapa pole wananchi wa Jimbo la Nyang’wale lakini pia kifuta machozi?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein, Mbunge wa Nyang’wale, kama Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuelezea changamoto hii ya fisi. Ni kweli kumekuwa na changamoto, fisi wanakuwa wamebaki kwenye maeneo ambayo siyo ya hifadhi na wamekuwa wakiwadhuru wananchi. Zoezi hili tulishaelekeza watendaji, pengine na hapa tena nitoe maelekezo kwamba watendaji walioko Kanda ya Mwanza, nikimaanisha magharibi tuandae operation ya kwenda kuwasaka wale fisi wote ambao hawako kwenye maeneo ya hifadhi na kuwarejesha kwenye maeneo ya hifadhi ili kunusuru hali za wananchi wa Jimbo la Nyang’wale. Ahsante. (Makofi)