Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salim Mussa Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza:- Je, ni nini kinachosababisha mabadiliko makubwa ya bei za tiketi za ndege za Air Tanzania kwa safari za Dar es Salaam na Dodoma ambapo mara nyingi hufika hadi shilingi laki sita?

Supplementary Question 1

MHE. SALIM MUSSA OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Miezi mitatu iliyopita Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi alipokea ndege pale Zanzibar; moja ilikuwa na jina la Tanzanite na nyingine ilikuwa na jina la Zanzibar; na aliahidi kwamba wataongeza miruko hadi Pemba: -

Je, ni lini Wizara hii itasukuma Shirika hili ili kuweza kufika Pemba? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salim Mussa Omar, Mbunge wa Gando kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekitk, kama Waziri alivyoahidi, ahadi hiyo ipo kwenye utekelezaji. Kwa hiyo, taratibu zote zitakapokamilika, ndege zitaanza kufanya safari kwenda Pemba.Ahsante.