Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi naomba nikiri majibu ya Serikali ni majibu mazuri sana ya kutia matumaini kwa wananchi wa Kalambo. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Tumaini la kuanza kujenga barabara hii limechukua muda mrefu na barabara hii itapita maeneo ambayo wananchi wanahitaji kupata fidia.

Swali la kwanza je, Serikali itakuwa tayari kuhakikisha kwamba kwa sababu imechukua muda mrefu unafanyika tathmini ili wananchi waweze kulipwa haki zao kwa mujibu wa kipindi cha leo?

Swali la pili je, Serikali imejiandaa kuanza kulipa fidia lini ili ujenzi ukamilike maana nimeambiwa kwamba iko kwenye vetting na AG namuona hapa naamini hata chelewesha katika hilo?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kandege kama ifuatavyo. Tutawalipa wananchi wote ambao watapitiwa na barabara kwa mujibu wa sheria Na. 13 ya mwaka 2007 Serikali itafanya hivyo.

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 2

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana barabara ya Mkomazi Kisiwani Same ambayo ina kilometa takriban 104 imekuwa inajengwa vipara vipara vya kilometa tano tangu mwaka 2006. Na barabara hii kwa hali hiyo inakuwa haina tija kwa wananchi ambao ile barabara inawagusa moja kwa moja. Je, Serikali inaweza ikawaambia nini wananchi haswa wa Jimbo la Same Mashariki ambao hii barabara ndio imekalia maendeleo yao?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Anne Malecela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kwamba barabara Mkomazi Same imechukua muda mrefu lakini hivi sasa Serikali tunajipanga kuhakikisha barabara hiyo inaendelea kujengwa kwa haraka zaidi kuliko hapo zamani hasa kwenye eneo lile la Same Mashariki ambako Mheshimiwa Anna Malechela yeye ndiyo Mbunge kule.

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 3

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru nina swali la nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi. Kipande cha barabara ya kutoka Uvinza mpaka Malagarasi kilometa 51 kiliahidiwa kujengwa tangu kwenye utawala wa Rais wa Awamu ya Nne Dkt Kikwete. Kipande hicho mpaka leo hakijaweza kujengwa lakini Chagu mpaka Kazilambwa nayo haijakamilika. Ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kipande hicho cha kilometa 51?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo. Barabara ya Uvinza Malagarasi yenye urefu wa kilomita 51 hivi sasa tuko kwenye mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya kumalizia kipande hicho ili sasa wananchi waweze kufaidi kutoka Dar es Salaam mpaka huko Kigoma barabara yote iwe na lami kwa asilimia 100.

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 4

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara hii. Kati ya wilaya kongwe zilizoko nchini Tanzania, ni pamoja na wilaya ya Masasi pamoja na wilaya ya Nachingwea. Hata hivyo wilaya ya Nachingwea na Masasi zinaungwanishwa kwa barabara yenye urefu wa kilometa 42, wilaya ile sasa ina miaka zaidi ya 50 kwa sababu ilikuwepo hata kabla ya uhuru na ilikuwa na jina lingine…

SPIKA: Uliza swali lako Mheshimiwa Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Sasa swali langu, ili kukuza uchumi wa Nachingwea tunahitaji barabara hii ijengwe kwa lami…

SPIKA: Uliza swali.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Ni lini Serikali itahakikisha barabara ya Nachingwea Masasi yenye urefu wa kilometa 42 inaunganishwa kwa lami?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mwambe kama ifuatavyo. Barabara Masasi Nachingwea yenye urefu wa kilometa 41 ni kweli ni barabara ya siku nyingi na sisi tunaitambua hivyo na tuko kwenye mpango wa kuhakikisha kwamba tunatafuta fedha ili tuweze kujenga kwa kiwango cha lami.

Name

Philipo Augustino Mulugo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songwe

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 5

MHE. PHILIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ni lini barabara ya kutoka Mbalizi hadi Mkwajuni mpaka Makongorosi itajengwa kwa kiwango cha lami kwa sababu ni wilaya mpya? Na wilaya zote za Songwe zina lami kasoro Songwe?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Philipo kama ifuatavyo. Barabara hii ni muhimu sana tunaijua ni barabara ambayo wanategemea wananchi wengi kwa ajili uchumi na sisi Serikali tuna mpango maalum wa kuijenga lakini tuko katika mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kuanzia Matai kwenda Kasesya border inayounganisha nchi yetu na nchi ya Zambia?

Supplementary Question 6

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuna barabara ya kutoka Mtwara pachani unapitia Kata ya Mkongo, Lusewa, Magazine hadi Nalasi Tunduru, je, ni lini Serikali itaijenga kwa kiwango cha lami barabara hii hasa ikichukuliwa maanani ishafanyiwa upembuzi yakinifu na pia iko katika Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Vita Kawawa kama ifuatavyo. Barabara hii aliyoizungumza ni barabara muhimu na ni barabara ndefu na kweli inahitajika kujengwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapitisha mazao yao bila matatizo Serikali tunao mpango wa kutafuta fedha na hivi karibuni naamini tutapata fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.