Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Daraja katika barabara ya Kishanda B limefunikwa na maji, hivyo kukatisha mawasiliano ya Wananchi wa kata za Nyaruzumbura, Nyakatuntu, Kakanja, Kikukuru, Mabila na Kitwe Wilayani Kyerwa. Je, ni lini Serikali itajenga Daraja katika barabara hiyo ili kuwarejeshea mawasiliano wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza niishukuru Serikali kwa kazi inayofanyika kwa upande wa barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kyerwa ni miongoni mwa Wilaya ambazo zina vipindi virefu vya mvua, barabara zake zinatengenezwa kwa udongo, sasa Serikali ina mpango gani wa kuongeza bajeti ili barabara hizi ambazo hazipitiki kipindi cha mvua ziweze kutengewa bajeti ya changarawe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; niishukuru Serikali kwa ombi langu lla kujenga lami katika Mji wa Nkwenda, kazi ambayo tayari imekamilika lakini nilileta ombi kwa sababu ya umuhimu wa ule Mji wa Nkwenda kuweka taa pale. Je, Serikali imefikia wapi ombi ambalo nimelileta kwenu kuweka lami katika Mji wa Nkwenda? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKLIA ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa
Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anaomba tu, amejaribu ni ombi vilevile ni ushauri, upi ni mpango wa Serikali wa kuongeza bajeti. Nafikiri baada ya Wabunge wengi kuzungumza ndani, Serikali katika bajeti kuu imekuja na mpango wa kuongeza fedha kwa TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tuseme tu kwa ongezeko hilo la fedha ambalo Bunge lako Tukufu likiwapendeza wakapitisha, basi tutaongeza bajeti katika halmashauri zote nchini ikiwemo Halmashauri ya Kyerwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili; ameshukuru kwamba Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa lami katika eneo la Mji wa Nkwenda na hiyo lami imeshakamilika lakini sasa hivi alileta ombi Serikalini na nimhakikishie tu kwamba ombi lake linatekelezwa na Serikali kwa sababu mkandarasi ameshapatikana, yupo site na taa zitawekwa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge kawaambie wananchi wa Kyerwa katika Mji wa Nkenda kwamba ombi ulilolileta basi linaanza kutekelezwa; hivi niavyozungumza mkandarasi amekwenda site, ahsante sana. (Makofi)