Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakuja na Mpango Madhubuti wa kuitumia Bahari kwa Programu za Uvuvi wa Bahari Kuu na michezo ya bahari ili kutengeneza ajira kwa Vijana wa Jimbo la Kawe, hasa ikizingatiwa nusu ya Jimbo hilo lipo Mwambao wa Bahari ya Hindi?

Supplementary Question 1

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza kwa kuwa, karibu wenyeji wote wa Jimbo la Kawe wanajishughulisha na shughuli za uvuvi mdogo mdogo hasa wa mitumbwi na mara nyingi hutokea ajali hasa wakati wa usiku na kuhatarisha wavuvi wetu. Ni lini sasa Serikali italeta Boti angalau Fiber Boat ndogo ndogo, kwa ajili ya kuokoa panapotokea madhila ya namna hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Kata ya Msasani, Kata ya Kawe, Kata ya Kunduchi, Kata ya Mbweni, Mbezi pamoja na Bunju yote hiyo ni wavuvi wadogo wadogo wanaotumia mitumbwi na mikopo ya halmashauri haiwapi nafasi kwa sababu ina ukomo wa miaka 35. Ni lini sasa Serikali itakuwa na mpango maalum wa kuwapa mikopo hawa wavuvi ili kusudi kuboresha uvuvi wao?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza ni kuhusu usalama wa wavuvi na uokozi pale wanapopata madhila mbalimbali baharini. Serikali kwa pamoja Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kupitia Police Marine lakini na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu zote zinafanya kazi kwa pamoja na hivi sasa ninavyozungumza, tuko katika mkakati wa kuhakikisha kwamba, panapatikana chombo au vyombo ambavyo vitakuwa vikifanya kazi hiyo ya doria na jambo hili linaratibiwa vyema na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa hivyo, wananchi wa Kawe na wenyewe wamo katika mpango wa namna hiyo.

Mheshimiwa Spika, Jambo la pili ni kuhusu mikopo. Mheshimiwa Askofu Gwajima, Mbunge wa Kawe nataka nikuhakikishie kwamba, tumejipanga vyema na katika bajeti yetu ya awamu hii ya 2021/2022 Serikali ya Awamu ya Sita ya mama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga vyema nataka nikukaribishe kwa ajili ya kuhakikisha vikundi na vijana wa pale Kawe waweze kupata mashine za boti lakini vilevile waweze kujiunga katika vikundi vitakavyowasaidia kutengeneza vichanja vya ukaushaji wa samaki na hata kutengeneza mashine za kuzalisha barafu wauziane wao wenyewe kwa ajili ya kuondosha tatizo la upotevu wa mazao. Ahsante.