Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Mradi wa Maji ambao ulishafanyiwa upembuzi yakinifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Nkome, Mchangani, Katome, Nyamboge, Nzera na Rwezera?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namshukuru pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali na wananchi wa Jimbo la Geita Vijijini wamekusikia. Hata hivyo, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa majibu haya sasa ni mara ya pili napewa katika katika Bunge lako Tukufu, namuomba Mheshimiwa Waziri yupo tayari sasa baada tu ya Bunge hili kuambatana nami kwenda kuona mazingira halisi ya wananchi wangu wanavyokaa ili aweze kutekeleza mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mradi huu unaishia katika Kijiji cha Idoselo, Vijiji vya Mkorani, Ibisabageni, Dubanga, Isulobutundwe vijiji ambavyo wananchi wake wanachota maji umbali wa kilometa tisa, 10 mpaka 20. Je, Wizara haioni umuhimu wa kunipatia angalau visima wakati wao wakisubiri mradi huu wa maji uende mpaka kwao?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunilinda suala la kuambatana na Mheshimiwa Musukuma lakini mara baada ya kutoa kibali hicho nitakuwa mtiifu kwako nitakwenda kutimiza majukumu yangu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusiana na visima, nimtoe hofu Mheshimiwa Musukumu tutakuja kuangalia hali halisi, wataalam wetu tutawaagiza wafike pale. Tumetenga visima vingi sana ili maeneo yote ambayo ulazaji wa mabomba unakuwa ni mgumu basi huduma ya visima vya maji iweze kupatikana. (Makofi)