Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kupeleka watumishi wa Idara ya Afya katika Jimbo la Kilwa Kaskazini ambalo lina uhaba mkubwa wa watumishi kiasi cha kufanya baadhi ya zahanati kutoa huduma duni na nyingine kuchelewa kufunguliwa?

Supplementary Question 1

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Hospitali ya Kipatimu ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi ya Kanisa Katoliki imekuwa na changamoto kubwa ya mtaalam wa mashine ya x-ray. Itakumbukwa kwamba mwaka 2017 Serikali ilitumia jumla ya shilingi milioni 60 kuleta mashine ya x-ray katika hospitali ile lakini mpaka leo hatujawa na mtumishi wa kitengo hicho.

Je, katika hizi ajira chache 2,726 ambazo zimetangazwa hivi karibuni, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kunihakikishia kwamba moja kati ya watumishi hao atapelekwa katika Hospitali ya Kipatimu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, je, Mheshimiwa Naibu Waziri au Waziri wa TAMISEMI lini atakuwa tayari kutembelea Wilaya ya Kilwa ili kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa? Ahsante.
(Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya, mwaka 2017 ilipeleka mashine ya x-ray na mpaka sasa utaratibu wa kumpata mtumishi kwa maana ya mtaalam wa x-ray upo hatua za mwisho na naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika ajira hizi ambazo tumezitangaza, tutakwenda kuhakikisha tunapata mtaalam wa x-ray kwa ajili ya kwenda kutoa huduma katika Hospitali ya Kipatimo.

Mheshimiwa Spika, lakini pili niko tayari kuambatana na Mheshimiwa Mbunge kufanya ziara katika Jimbo la Kilwa mara baada ya kumaliza session hizi za Bunge Juni 30, 2021. Ninakushukuru sana. (Makofi)