Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imekumbwa na wimbi kubwa la uvamizi wa wanyamapori kwenye maeneo ya vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa na Hifadhi ya Wanyamapori Makao na kusababisha uharibifu wa mazao na kutishia usalama wa watu. (a) Je, ni lini Serikali itashughulikia tatizo la uhaba wa watumishi wa Idara ya Wanyamapori? (b) Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi vikiwemo gari na silaha?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nakushuru na ninaishukuru Serikali kwa kuleta shilingi milioni 51 kwa ajili ya kulipa fidia na kifuta machozi.

Je, ni lini Serikali italeta muswada Bungeni wa kuongeza viwango vya kifuta machozi pamoja na fidia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na watumishi wa Idara ya Wanyamapori Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ambao ni wawili tu wameelemewa kutokana na upungufu wa vitendea kazi.

Je, Serikali haioni kwa kipindi hiki cha miezi miwili watumishi wa TAWA wakawepo doria wakati wa usiku ili kusaidiana na wananchi wanaokesha ili wananchi waweze kuvuna mazao yao katika kipindi hiki? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Uatlii naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Leah Komanya, Mbunge wa Meatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nianze na hili la pili; ninaomba nimuahidi Mbunge na Wabunge wengine wote ambao wana changamoto ya tembo kwamba kipindi hiki ambacho ni cha mavuno, askari watasimamia zoezi mpaka pale ambapo wananchi watatoa mazao yao na hili litaanza kuanzia sasa. Nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge hili tutalitekeleza sisi kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili la kwanza ambalo alisema kuleta muswada wa kuongeza kifuta machozi na kifuta jasho kwa wale ambao wameathirika na wanyama wakali hususan tembo; nimelipokea lakini wakati huo huo Serikali inaendelea kuangalia tathmini ya namna ya kufanya, lakini wakati huo huo tunaangalia nchi zingine wamefanyaje.

Mheshimiwa Spika, suala hili kwenye nchi za wenzetu/ majirani zetu ambao wana changamoto kama hii, wao liliwashinda wakaamua kuachana na mambo ya kifuta machozi kwa sababu kadri changamoto inavyozidi kuongezeka, ndivyo gharama zinavyozidi kuongezeka. Serikali ya Tanzania kwa kuwathamini wananchi wake iliona bora iweke hili eneo ili angalau wananchi waweze kufaidika. Kwa hiyo, tunalipokea lakini tutaenda kulichakata na tuone faida na hasara kwa pande zote mbili, ahsante. (Makofi)

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imekumbwa na wimbi kubwa la uvamizi wa wanyamapori kwenye maeneo ya vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa na Hifadhi ya Wanyamapori Makao na kusababisha uharibifu wa mazao na kutishia usalama wa watu. (a) Je, ni lini Serikali itashughulikia tatizo la uhaba wa watumishi wa Idara ya Wanyamapori? (b) Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi vikiwemo gari na silaha?

Supplementary Question 2

MHE.CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona na kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba idadi ya watu nchini inaongezeka, lakini ardhi tuliyonayo haiongezeki na yapo mapori kama hayo na mengine ambayo kwa namna moja ama nyingine hayana tija kwa Taifa.

Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kufanyia tathmini mapori mengine kuyagawa kwa wananchi ili waweze kuyatumia?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maliaisli na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Paresso, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inapokea mawazo hayo na hata sasa kwa sababu kuna changamoto na migogoro mingi kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi, Serikali inaendelea kufanya tathmini na yale maeneo ambayo yanaonekana sio ya faida sana, Serikali itaangalia na italeta mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri na mwisho Mheshimiwa Rais atatoa maelekezo, ahsante. (Makofi)

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imekumbwa na wimbi kubwa la uvamizi wa wanyamapori kwenye maeneo ya vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa na Hifadhi ya Wanyamapori Makao na kusababisha uharibifu wa mazao na kutishia usalama wa watu. (a) Je, ni lini Serikali itashughulikia tatizo la uhaba wa watumishi wa Idara ya Wanyamapori? (b) Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi vikiwemo gari na silaha?

Supplementary Question 3

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.

Mheshimiwa Spika, haya mambo ya wanyamapori mimi naona kwamba sasa tunapokwenda tutabakiza nchi ya wanyamapori. (KIcheko)

Sasa mimi najiuliza hivi ni tembo wangapi wanatosha kuishi katika mapori ya Tanzania ambayo watalii watakuja kuona, kwa sababu kama tembo hawa hawana uzazi wa mpango maana yake sasa tuwaruhusu waishi kwa wananchi, ni tembo wangapi wanatosha ili watalii waone kwamba hawa tembo wametosha tunakwenda kuwaona. Maana yake tunapoamini tembo wakiwa wachache ndio watalii watawatafuta, sasa wakiwa wengi … kwenye utalii gani?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa Getere, Mbunge wa Bunda Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nimpe tathmini ya idadi ya tembo mpaka sasa; mwaka 2009 kulikuwa na idadi ya tembo 134,000 lakini kabla ya hapo walikuwa wanafika tembo 300 na kadhalika, lakini walishuka mpaka kufikia 134,000. Toka mwaka 2009 mpaka 2014 ambapo kulikuwa na poaching kubwa, tembo walishuka mpaka wakafika 43,000. Kutoka mwaka 2014 mpaka 2020 wanakadiriwa sasa
wameongezeka kufika 60,000.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, utaangalia hata ile idadi ya mwaka 2009 bado hatujaifikia; kinachotokea hapa ni kwamba tembo anahamasika hasa kipindi cha mavuno, anaweka kambi kwenye maeneo ambayo ni shoroba zao na anapoweka ile kambi basi wanahamasika kula mazao ambayo pengine huyu tembo toka azaliwe hajawahi kukutana na hindi, muhogo anahamasika ndiyo maana sasa changamoto sasa hivi imekuwa ni kubwa kwa sababu ni kipindi hiki hasa cha mavuno, ahsante.