Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO K.n.y. MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza:- Idadi ya watu wa Same imekuwa ikiongezeka tangu tupate Uhuru na mpaka wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi upo kilometa tatu kutoka Same Mjini. Wanyamapori na hasa tembo wameonekana Same Mjini mara nyingi. Je, ni lini Serikali itafikiria kuweka upya mipaka mipya ya hifadhi ili kutoa maeneo kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli nyingine za kijamii?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri na juhudi za Wizara ambazo tunaziona, lakini kwa kuwa mipaka ya hifadhi hii iliwekwa mwaka 1954 na idadi ya watu imezidi kuongezeka kiasi kwamba sasa hivi Makao Makuu ya Mji Mdogo wa Same yapo kilometa nne tu kutoka kwenye mpaka wa hifadhi.

Je, Serikali haioni kwamba suala la eneo hili la Same Magharibi lichukuliwe kama special case ili kuwapa watu nafasi ya kuweza kufanya kazi zao kwa sababu mpaka upo karibu sana na Makao Makuu ya Mji Mdogo wa Same? Ahsante.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Malisisli na Utalii naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tadayo, Mbunge wa Mwanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, ni kwamba Same ipo kilometa sita kutoka maeneo ya makazi ambayo wanaishi wananchi mpaka kwenye eneo la hifadhi. Kama ambavyo nimeelezea kwamba sasa hivi tuna changamoto ya tembo na hawa tembo wanarudi kwenye maeneo yao ya zamani, kwa hiyo, kuendelea kumega hili eneo ni kuendelea sasa kuongeza migogoro kati ya wananchi na wanyama.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge kwamba wakati Serikali inaangalia utaratibu mwingine basi wananchi waendelee kuishi kwenye maeneo hayo kuliko kuendelea kuwasogeza kwenye hatari zaidi kuliko ilivyo sasa, ahsante.

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO K.n.y. MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza:- Idadi ya watu wa Same imekuwa ikiongezeka tangu tupate Uhuru na mpaka wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi upo kilometa tatu kutoka Same Mjini. Wanyamapori na hasa tembo wameonekana Same Mjini mara nyingi. Je, ni lini Serikali itafikiria kuweka upya mipaka mipya ya hifadhi ili kutoa maeneo kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli nyingine za kijamii?

Supplementary Question 2

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwa kweli wakazi wengi wa Same ambao wanaishi karibu na Mkomazi National Park wapo kwenye risk kubwa ya kupata matatizo na kupoteza maisha yao. Kwa sababu Mheshimiwa Waziri tulikuwa naye Jumamosi na Jumapili kule Same na ameona hali ilivyo, haoni kwamba ni vyema zile sehemu zote ambazo zina risk kubwa kukawepo askari ambao wanakuwepo kuwafukuza wale tembo kuliko kuacha hali ilivyo mpaka sasa? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anne Kilango, Mbunge wa Same Mashariki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tulienda ziara na Mheshimiwa Anne Kilango, changamoto ya tembo ipo, ni kweli na ni kubwa, lakini tulitoa maelekezo na naomba hili niendelee kuelekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba tutaweka kambi ambazo zitakuwa ni za doria kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanaishi kwa usalama.

Mheshimiwa Spika, na hili nikuahidi kwamba maeneo yote ambayo yana risk kubwa ya tembo, tutahakikisha kwamba askari wanaishi maeneo yale ili changamoto hii hasa kipindi hiki cha mavuno tuweze kuidhibiti na wananchi waishi kwa amani, ahsante. (Makofi)