Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ili ifahamike kwa Watalii wa ndani na nje?

Supplementary Question 1

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza: kwenye Hifadhi ya Kitulo kwa sababu ni hifadhi yenye upekee na hifadhi nyingine za Tanzania: Je, Serikali haioni haja kuwavutia zaidi wawekezaji kwa kupunguza gharama za uwekezaji; kwa sababu, gharama zimekuwa ni kubwa? Kwa maana, ukiangalia kuna wana- Makete na Watanzania ambao wako tayari kuwekeza kwenye hifadhi hizi, lakini gharama kwa mfano za environmental assessment tu ni zaidi ya shilingi milioni 50, kitu ambacho kimekuwa kiki-discourage wawekezaji.

Sasa je, Serikali umuhimu wa kupunguza gharama ili wawekezaji wawe wengi kwenye hifadhi zetu na ziweze kutangazwa?

Swali la pili: Hifadhi ya Kitulo inaenda kupitiwa na barabara ya kiwango cha lami inayotoka Isyonje kwenda Kitulo kupitia Makete, lakini bado miundombinu ya ndani ya hifadhi siyo mizuri kwa maana ya barabara: Ni mpango upi wa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili kuhakikisha kwamba miundombinu ndani ya Hifadhi ya Kitulo inaimarishwa ili tuweze kuvutia wawekezaji wengi zaidi? Ahsante.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa
Naibu Spika, ahsante. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Sanga kwa kuwa na jitihada nyingi sana za kuhakikisha kwamba hifadhi yetu ya Taifa ya Kitulo inapaishwa vizuri, hasa kiuwekezaji, lakini pia kwenye maeneo ya utalii. Napenda nimweleweshe Mheshimiwa Mbunge kwamba, sisi kama Wizara ya Maliasili na Utalii hatuna gharama yoyote inayohusiana na uwekezaji. Wawekezaji wa aina mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanaalikwa kwenye maeneo yote ya uhifadhi kuja kuwekeza uwekezaji mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa hoteli, ma-tent, camps, hostels mpaka na lodge. Sisi tunawaalika wawekezaji wote bila kubagua. Gharama kama gharama ni taratibu za uwekezaji ambazo haziko kwenye Wizara yetu, isipokuwa mwekezaji yeyote anatakiwa kufuata.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande wa miundombinu Serikali imejipanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuhakikisha kwamba maeneo yote ya uhifadhi yanatengewa fedha ya kutosha kuhakikisha miundombinu yote ndani ya hifadhi inaimarika vizuri ili kwenye upande wa utalii sasa tuweze kuhamasisha utalii na maeneo yale yaweze kupitika kwa urahisi. Ahsante.

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ili ifahamike kwa Watalii wa ndani na nje?

Supplementary Question 2

MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni hitaji la wananchi wa Kitulo la kuitangaza hifadhi hiyo kama kivutio ambacho kiko nchini kwetu; na kwa kuwa, hitaji hilo linafanana sana na hitaji la wananchi wa Katavi la kuitangaza Katavi National Park ambayo ina vivutio vingi sana vya asili vya utofauti akiwepo twiga mweupe anayepatikana kipekee sana katika Mkoa wetu wa Katavi:-

Je, Serikali ina mikakati gani mipya ya kuitangaza hifadhi hiyo ili iweze kufahamika ndani na nje ya nchi?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa
Naibu Spika, ahsante. Serikali ina mpango wa kuipaisha hifadhi ya Katavi kwa kuzingatia bajeti iliyopo kwenye mwaka wa fedha wa 2021/2022. Eneo hili ni eneo zuri sana kwenye upande wa utalii.

Mheshimuwa Naibu Spika, hivyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Martha kwamba Serikali inatambua mchango wa Hifadhi ya Katavi na kwamba ni eneo zuri sana kwenye kuhamasisha utalii. Hivyo, tutajitahidi sana pamoja na maeneo mengine yote yaliyoko Tanzania ambayo yana vivutio kuhakikisha kwamba tunayatangaza ili tuweze kupata watalii wengi na kufikia namba ambayo imekusudiwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.