Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Muhammed Amour Muhammed

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Bumbwini

Primary Question

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED aliuliza:- Kumekuwa na unyanyasaji mkubwa unaofanywa na JWTZ wa kuwanyang‟anya wavuvi samaki wao licha ya kwamba watu hao wanajitafutia kipato kupitia bahari kama Watanzania. Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa unyanyasaji huo unaofanywa na Jeshi la Wananchi kwa wananchi wake?

Supplementary Question 1

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED: Mheshimiwa Spika, ahsante sana pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri lakini pia sikuridhika sana na majibu yake ambayo ameyatoa ya kubahatisha zaidi. Tunao ushahidi wa kutosha kabisa mpaka wahanga waliopigwa na kunyang‟anywa samaki wao wavuvi na JW (Jeshi la Wananchi) sasa sijui Mheshimiwa Waziri na kisingizio hapa ni license zinazotumika wanadai kwamba sizo.
Mheshimiwa Spika, sasa swali langu la kwanza katika swali la nyongeza ni aina gani ya license zinazotakiwa kutumika na wavuvi hawa?
Swali la pili, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana na mimi tukamuonesha wale wahanga ambao walipigwa na wakati mwingine walinyang‟anywa samaki wao, matendo haya yanafanyika zaidi katika bahari ya Kigamboni na Kunduchi? Ahsante sana.

Name

Dr. Hussein Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, kwanza niseme kwamba niko tayari kufuatana na Mheshimiwa Mbunge kwenda kuwaona hao ambao inasemekana ni wahanga wa kipigo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini napenda nirudie yale niliyoyasema kwenye jibu langu la msingi kwamba kwa kuwa nchi hii inafata utawala wa sheria ni vema basi Mheshimiwa Mbunge anapopata tuhuma kama hizo akazifikisha sehemu husika.
Mheshimiwa Spika, siyo vema suala kama hili tulisikie mara ya kwanza ndani ya Bunge, sisi tupo, ofisi zetu zipo, Mheshimiwa Mbunge alipaswa kutufikishia ili tufanye uchunguzi na pale inapothibitika tuchukue hatua stahili, ningependa tuende kwa mwendo huo zaidi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu ni aina gani za leseni niseme tu kwamba hili ni suala ambalo liko chini ya Wizara inayohusika na masuala ya uvuvi. Wanajeshi wanajukumu moja la kuhakikisha kwamba wavuvi hawatumii njia za uvuvi wa haramu basi, siyo suala la kuangalia leseni, leseni ina mamlaka zake.
Mheshimiwa Spika, hivyo, tunachoweza kusema hapa ni kwamba yanapotokea matukio kama haya toa taarifa ili tufanye uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahili.