Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, ni lini utekelezaji wa mradi wa kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Serikali. Naomba niulize maswali madogo mawili. Kutokana na Mradi huu wa REGROW tulitegemea sasa wananchi wa Mikoa ya Kusini kuanza kutengeneza ajira nyingi sana kupitia utalii na kuongeza pato la mikoa hii; na tulitegemea sasa ujenzi wa Vyuo vya Utalii Nyanda za Juu Kusini katika eneo la Kihesa Kilolo na Makao Makuu.

Je, ni elimu kiasi gani imetolewa kwa wananchi wa mikoa hii ili kuwajengea uwezo katika kuupokea mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Biashara ni matangazo. Kwa kuwa mikoa yetu hii ya kusini tunavyo vivutio vingi na vizuri vikiwemo Mbunga za Wanyama Ruaha National Park ambapo ni Mbuga ya pili kwa ukubwa katika Afrika; tunavyo vivutio vingine kwa mfano pale Kihesa kuna Gangilonga, jiwe lililokuwa linaongea, lakini tuna Kitanzini ambayo ni sehemu ambayo watu walikuwa wanajinyongea; na vile vile tunalo fuvu la Mtwa Mkwawa ambalo lipo pale Kalenga…

SPIKA: Sasa swali Mheshimiwa.

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nini mkakati wa kuvitangaza hivi vivutio vya kusini ili kupata angalau tupate watalii wa ndani na kuongeza mapato? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Ritta kwa swali lake zuri, maana hii ni kwa manufaa ya Mikoa yote ya Kusini mwa Tanzania. Mradi huu ni faida kubwa sana kwa wananchi na mikoa ya kusini mwa Tanzania kwani Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha ambao ni mkopo.

Mheshimiwa Spika, katika swali la msingi la Mheshimiwa Ritta ameuliza kwamba tuna mkakati gani kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha pindi wanapopokea huu mradi? Pia na namna ambavyo wataenda kutelekeleza.

Mheshimiwa Spika, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina mpango mkubwa wa kuanzisha vyuo ambavyoo vitakuwa ni campus. Tunaanzisha campus ya Mweka na pia kutakuwa na Chuo cha Mambo ya Utalii ambacho kitaanzishwa kama Campus ya Iringa. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi kwamba wananchi wa kusini mwa Tanzania wataweza kuelimika. Pia tutahamasisha utalii kupitia elimu hiyo.

Mheshimiwa Spika, swali lake lingine alisema biashara ni matangazo. Ni kweli bila kutangaza vivutio vyetu tulivyonavyo hapa nchini, utalii hauwezi kuendelea. Kipindi cha mpango huu wa bajeti, tumetenga kiasi cha shilingi bilioni 46.5 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba utangazaji wa vivutio tulivyonavyo hapa nchini unafanyika kwa nguvu zote.

Mheshimiwa Spika, pia kwenye utangazaji bila kuimarisha miundombinu inakuwa ni changamoto; na hilo nimtoe wasiwasi kwamba tumetenga shilingi bilioni 75.4 ambazo zitaimarisha miundombinu iliyoko kwenye hifadhi hizo ili tuimarishe na kutangaza kwa bidii. Ahsante. (Makofi)