Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatoa eneo la Hifadhi ya Bonde la Wembere kwa Wananchi wa Igunga kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo na ufugaji ili kumaliza mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo kwa kuwa Bonde hilo limepoteza sifa ya kuwa Hifadhi?

Supplementary Question 1

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru majibu ya Serikali, lakini kwa kuwa, mgogoro huu umekuwa ni wa muda mrefu na umechukua eneo kubwa la Jimbo la Igunga, takribani kilometa za mraba 450. Sasa nilikuwa namuomba Naibu Waziri kwasababu, kumekuwa pia kuna mvutano kati ya wananchi na Serikali na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya yetu, nilikuwa namuomba Naibu Waziri kama atakuwa tayari baada ya Bunge hili la Bajeti niambatane naye tuende Igunga tukakutane na wananchi na Kamati ya Ulinzi na Usalama tuweze kulimaliza? Ahsante.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTALII NA MALIASILI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaomba tushirikiane Waheshimiwa wote Wabunge ambao tunawakilisha wananchi kutoka katika maeneo yetu husika. Suala muhimu la uhifadhi ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua kwamba, Serikali inapohifadhi maeneo husika ni kwa ajili ya faida ya wananchi wa eneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia jibu langu la msingi ambalo nimelijibu mwanzo, nimeelezea kwamba, eneo hili ni moja ya vyanzo vya maji ambavyo vinategemewa katika Mikoa ya Tabora, Simiyu na Singida.

Kwa hiyo, ninakubaliana na wazo la Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaambatana naye, lakini ni wajibu wa kila Mheshimiwa kuelimisha wananchi wanaomzunguka kwamba, uhifadhi ni wajibu wa kila mtu na faida na hasara za uhifadhi tunaziona, lakini pia tunapohifadhi vyanzo hivi vya maji ni kwa ajili ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo husika. Lakini pia tunaepuka mambo mengi ikiwemo kuanzisha majangwa ambayo yanaweza yakasababisha ukame katika nchi yetu. Naomba kuwasilisha.