Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUDITH S. KAPINGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutenganisha fedha za maendeleo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Fedha za Bodi ya Mikopo kwa kuzitengea Vote tofauti fedha hizi za mikopo ili kuleta tija ya miradi ya maendeleo?

Supplementary Question 1

MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza napenda kuishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini napenda kuwashukuru kwa kuongeza rasilimali fedha katika miradi ya maendeleo ya Wizara. Nina swali dogo la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Fedha katika Bunge la Bajeti la 2019/2020 ilitoa maelekezo kwa Bodi ya Mikopo kuangalia uwezekano wa kufanyia kazi suala hili. Je, Wizara haioni umuhimu wa kufanyia kazi mapendekezo haya ya Wizara ya Fedha ili shughuli hii ya kuendeleza mitaji watu kama Wizara inavyosema iweze kufanyiwa kazi vizuri kwa kuitenganisha na Fungu 46? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Judith, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile ilikuwa ni mapendekezo na yalipendekezwa na Wizara ya Fedha na kwa vile yalikuwa ni mapendekezo ambayo yaliletwa kwenye Wizara yetu, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa mapendekezo hayo tutaendelea kuyafanyia kazi na pale muda muafaka utakapofika tutawasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu. Ahsante.