Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ezekiel Magolyo Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. EZEKIEL M. MAIGE aliuliza:- Kwa kuwa Serikali imekuwa ikiwarasimisha wachimbaji wadogo wa madini:- (a) Je, ni lini Serikali itawarasimisha Wachimbaji wadogo katika vijiji vya Busulwangili, Lwabakanga, Kakola namba Tisa na Wisolele katika Jimbo la Msalala? (b) Je, ni sawa kwa mwenye leseni au msimamizi wa eneo la wachimbaji wadogo kupatiwa asilimia 30 ya mawe yanayochimbwa katika eneo lake?

Supplementary Question 1

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali ilielekeza wananchi waunde vikundi vya uchimbaji ili wasimamie rush wenyewe, je, ni kwa nini sasa Kamishna wa Madini Kahama anaweka wasimamizi ambao si wanavikundi na utaratibu gani unatumika kuwapata wasimamizi hao?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa nini eneo la Wisolele limetolewa leseni kwa watu binafsi akiwemo mtu mmoja ambaye anajinasibu kuwa karibu na viongozi wa tume (jina nalihifadhi) aliyepata leseni zaidi ya 17 peke yake badala ya vikundi vya wachimbaji wadogo kama Waziri alivyojibu kwenye jibu la msingi?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbunge wa Msalala, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la swali la msingi kuwa, Serikali kupitia Tume ya Madini ilitoa Waraka wa Ndani Na.3 ulioanza kutumika tarehe 15 Oktoba, 2019, wenye dhumuni la kutoa mwongozo kwa Maafisa Madini Wakazi na watumishi wengine katika kusimamia, kudhibiti shughuli za madini na mapato ya Serikali katika maeneo yenye rush. Kwa mujibu wa Waraka huo Afisa Madini Mkazi ni Mwenyeketi wa Kamati ya Uongozi unaofuatilia na kuimarisha usimamizi katika eneo la rush. Kamati hiyo inajumuisha DSO (Katibu), TAKUKURU (Mjumbe), OCD (Mjumbe), REMA (Mjumbe) na Halmashauri (Mjumbe).

Mheshimiwa Spika, utaratibu unaotumika kuwapata wasimamizi wa rush ni kupitia Kamati ya Uongozi unaofuatilia na kuimarisha usimamizi katika eneo la rush kama ilivyotajwa hapo juu. Kamati hiyo huteua Wasimamizi wa rush, ambapo Mwenyekiti wa rush anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-

Awe mchimbaji mzoefu hasa katika usimamizi wa maeneo ya aina hiyo; awe hana historia ya wizi wa fedha za Serikali na awe mwaminifu. Wajumbe wengine kwenye usimamizi wa rush ni pamoja na Katibu, Mweka Hazina, Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Mjumbe wa REMA, TAWOMA, mwakilishi wa eneo/shamba.

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika eneo la Wisolele zimetolewa leseni za uchimbaji mdogo 55 kwa watu binafsi na vikundi mbalimbali. Aidha, kuna jumla ya maombi ya leseni za uchimbaji mdogo 95. Kati ya maombi hayo, maombi sita ni ya vikundi vya Amani Gold Mine, Chapakazi, Domain Gold Group na Pamoja Mining Group.

Mheshimiwa Spika, utolewaji wa leseni hizo 55 ukijumuisha leseni 17 zilizotajwa na Mheshimiwa Mbunge zilitolewa kabla ya rush na vikundi kuundwa. Kwa mujibu wa Sheria ya Madini, 2010 pamoja na Marekebisho yake ya 2017 mchimbaji mdogo hazuiwi kumiliki leseni zaidi ya moja.