Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Othman Omar Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. OTHMAN OMAR HAJI aliuliza:- Lengo kuu la Mpango wa Kujithathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM) ni kuziwezesha nchi za Afrika kuimarisha utawala bora kwa kuwawezesha wananchi wake kubainisha changamoto:- Je, ni hatua gani ambazo zinachukuliwa na Tanzania katika kutekeleza mpango huo?

Supplementary Question 1

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa mujibu wa maelezo ya Serikali ni kwamba APRM Tanzania inafanya shughuli zake chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sababu hiyo basi, itawezaje kuisimamia Serikali na kutoa majibu yaliyo sahihi kwa wananchi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, moja kati ya masharti ya APRM kwa wanachama wake ni kwamba mwanachama anatakiwa akubali kufanyiwa tathmini na wanachama wenza. Je, ni mara ngapi Serikali ya Tanzania imewahi kufanyiwa tathmini hii na wanachama wenzake?

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza Mheshimiwa Othman Omar Haji, Mbunge wa Gando kwa maswali yake mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ukisoma mkataba ambao umeanzisha APRM, inaongozwa na Baraza la Usimamizi la Taifa ambalo ni huru, linachaguliwa kutoka kwa watu mbalimbali, asasi za Kiserikali, vyama vya kisiasa na watumishi wa upande wa Serikali. Baraza hilo ni huru katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha mkataba huo na kwamba iko chini ya Wizara lakini muundo na utendaji wake unawahakikishia kwamba baraza hilo liko huru na wala haliwezi kuingiliwa na mtu yeyote.

Mheshimiwa Spika, swali la pili la kuweza kuhakikiwa au kufanyiwa tathmini na wanachama wenza. Naomba tu nimkumbushe Mheshimiwa Othman Omar Haji kwamba APRM ilianzishwa na nchi za Kiafrika ili kuweka viwango vya kujitathmini ambavyo vinakubalika na Afrka na nchi za Kiafrika. Kwa hiyo, Tanzania imeruhusu nchi nyingi za Afrika, SADC na Afrika Mashariki kuweza kushiriki kwenye tathmini na kuweza kuzitathmini kwa mara nyingi zaidi. Ahsante.