Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Kituo cha Afya kilichopo Kigoma Ujiji Manispaa kinahudumia wakazi zaidi ya elfu arobaini katika Kata kumi na moja za Manispaa lakini kina kinakabiliwa na ukosefu wa Chumba cha theatre, X-ray pamoja na Ultra Sound:- Je, ni lini Serikali itakipatia Kituo hiki vifaa hivyo ili kusaidia wananchi hao wanaohudumiwa na Kituo hicho?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwanza niishukuru Serikali pale Rombo nina Kituo cha Afya kinaitwa Kituo cha Karume, tulipewa shilingi milioni 500 kwa hiyo ni kimekuwa kituo cha afya cha kisasa kabisa sasa hivi. Hata hivyo vipo vituo ambavyo havina kabisa vifaa vya hospitali, na tuna upungufu wa wahudumu wa afya takriban asilimia 58 ya wahudumu wanaotakiwa kuwepo?

Je, Serikali iko tayari kutusaidia ili vituo vingine hivi viweze kupata vifaa ili kusaidiana na ile hospitali ya wilaya katika kuhudumia wagonjwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema tuna shida kubwa sana ya watumishi wa afya; asilimia 58 ya watumishi wanaotakiwa wawepo, hawapo, je katika mgao Serikali iko tayari kufikiria kutupatia mgao wa watumishi wa afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru; naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Joseph Roman Selasini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa wa niaba ya Wizara nipokee pongezi, Mheshimiwa Selasini anasema kituo chake ambacho amepata jumla ya shilingi milioni 500, ni miongoni mwa vituo vya kisasa kabisa nchini. Naomba nitumie fursa hii kuwataarifu Waheshimiwa Wabunge Vituo kama hicho anachokisema Mheshimiwa Selasini viko vimejengwa nchini nzima. Kwa hiyo ni pongezi ambayo inatustahili Serikali kuweza kuipokea kwa sababu ni kazi kubwa ambayo imefanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake anaongelea suala zima la vifaa; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine wote ambao vituo vya afya vimejengwa kwenye maeneo yao, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba vile vituo vyote ambavyo vimejengwa havibaki vikawa ni mapambo, vinatakiwa vikamilike na vipelekewe na vifaa. Hivi ninavyoongea kuna kiasi cha fedha takribani bilioni 40 ambazo tunazifatilia Hazina ili tuweze kuhakikisha kwamba vifaa vinanunuliwa na vinapelekwa vituo vyote vya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili, anaongelea juu ya umuhimu wa watumishi. Ni kweli, tukiweka vifaa bila kuwa na watumishi napo itukuwa hatujafanya lolote. Naomba nitumie fursa hii kumtaarifu yeye pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine wote kwamba katika maombi tumeomba kupatiwa watumishi 12,000 na ni imani yetu kwamba maeneo yatakayozingatiwa ni yale ambayo yana upungufu mkubwa ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Roman Selasini.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Kituo cha Afya kilichopo Kigoma Ujiji Manispaa kinahudumia wakazi zaidi ya elfu arobaini katika Kata kumi na moja za Manispaa lakini kina kinakabiliwa na ukosefu wa Chumba cha theatre, X-ray pamoja na Ultra Sound:- Je, ni lini Serikali itakipatia Kituo hiki vifaa hivyo ili kusaidia wananchi hao wanaohudumiwa na Kituo hicho?

Supplementary Question 2

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika Ilani yake ilieleza kwamba itatoa matibabu bure kwa wazee, kwa Wilaya ya Nyang’hwale kuna wazee takribani 6,000 na wazee hawa ni 100 tu ambao wanapata matibabu bure, Je, Waziri ananiambia nini? Hawa wazee 5,900 waliobaki watapata vitambulisho vya kuweza kupata matibabu bure?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amar kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwanza, naomba tukubaliane naye kwamba si wazee wote ambao tumeahidi kuwapa matibabu bure, tumeahidi kutoa matibabu bure kwa wale wazee ambao hawana uwezo, kwa hiyo hilo lazima tuwekane sawa. Na ni ahadi ambayo iko thabiti baada ya kufata procedure zote ambazo zinatakiwa tunaamini kabisa wazee hawa wamefanya kazi kubwa katika kutumikia taifa hili la Tanzania ndiyo wametufikisha hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba wale wote ambao hawana uwezo wanatibiwa bure kama ambavyo sera ya Serikali inavyoelekeza. (Makofi)

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Kituo cha Afya kilichopo Kigoma Ujiji Manispaa kinahudumia wakazi zaidi ya elfu arobaini katika Kata kumi na moja za Manispaa lakini kina kinakabiliwa na ukosefu wa Chumba cha theatre, X-ray pamoja na Ultra Sound:- Je, ni lini Serikali itakipatia Kituo hiki vifaa hivyo ili kusaidia wananchi hao wanaohudumiwa na Kituo hicho?

Supplementary Question 3

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Tuna Zahanati iko katika Kata ya Luhunga Kijiji cha Igoda, ile zahanati tulishamaliza kujenga kila kitu na vitanda tulishaweka, na sasa ina miaka miwili haijafunguliwa. Je, ni lini Serikali sasa itaenda kufungua ile zahanati ambayo imejengwa na wananchi ili iweze kuanza kufanya kazi?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa maelekezo kwa Waganga wote wa wilaya nchini, kwamba maeneo ambayo wananchi wamejenga zahanati na zimekamilika hakuna sababu ya kuendelea kusubiria zisianze kutoa huduma; na hasa pale anaposema Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari vifaa vyote vipo. Kwa hiyo ni vizuri ndani ya Wilaya wahakikishe kwamba wanapeleka watumishi; kazi ambayo inawezekana kabisa; ili zahanati hiyo ianze kufanya kazi na wananchi wafaidi matunda ya jasho lao.