Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DEVOTHA M. MINJA (K.n.y. MHE. SUSAN L. KIWANGA) aliuliza:- Kata za Mchombe, Igima, Mbingu, Namwawala na Idete katika Jimbo la Mlimba zilipelekewa mradi wa umeme kwa gharama nafuu lakini mradi huo umefanywa vibaya na hivyo kusababisha wananchi wengi kukosa umeme:- (a) Je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwa wananchi hao? (b) REA ilikabidhiwa mkandarasi kupima maeneo yatakayounganishwa umeme katika vijiji vya Msolwa, Miembeni, Iduimdembo, Ipungusa, Matema, Lumumwe, Uchindile, Kitete na Ngwasi katika Awamu ya Pili; Je, kwa nini kazi hiyo inasuasua?

Supplementary Question 1

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nimesikiliza majibu ya Serikali kwa namna zoezi hili linavyokwenda kwa kusuasua hivi, Serikali itafanya juhudu gani za ziada ili ifikapo Juni, 2020 kama alivyosema Naibu Waziri kwamba umeme huo umefika katika Vijiji vya Ipungusa, Msolwa, Kalengakule, Miembeni, Iduindembo, Ipungusa, Matema, Lumumwe, Uchindile, Kitete, Idandu na Mgwasi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika Manispaa ya Morogoro zipo kata ambazo hazina umeme licha ya kuwepo mjini, kata hizi ni Kauzeni Juu, Kiegea, maeneo ya Mkundi, Magadu Juu, katika Kata ya Tungi maeneo ya Paranganyiki, Kambi A, na B; Je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwa wananchi hao?

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Devotha Minja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Devotha Minja ameulizia ni namna gani Serikali itafanya kuhakikisha ifikapo Juni, 2020 kwamba umeme maeneo hayo yaliyotajwa katika swali la msingi yanapatiwa umeme. Naomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kulikuwa na kusuasua kwa mkandarasi State Grid katika Mkoa wa Morogoro lakini hivi ninavyosimama ndani ya Bunge naomba nimtaarifu kwamba kwa wiki ijayo kwanza kwa sasa alishawasha vijiji 18 kati ya 150 katika Mkoa Morogoro; na kwa kuwa kulikuwa na tatizo la nguzo, alikuwa na nguzo zaidi ya 900 ambazo zilivyopimwa zilionekana kama haizifai. Ninapozungumza ndani ya Bunge zaidi ya nguzo 700 zimeonekana zinafaa sasa zinaweza zikaendelea na mradi na wiki ijayo anapokea nguzo 2,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, wiki ijayo atawasha vijiji 16 vikiwemo 6 vya Wilaya ya Kilombero vikiwemo alivyovitaja ambavyo ni Kilama, Kalengakelu, Matema, Iduendemo, Miembeni na Msolwa. Vijiji hivi vitawashwa wiki ijayo na mimi natarajia kufanya ziara katika Mkoa wa Morogoro, tutamwalika Mheshimiwa Mbunge tuambatane pamoja. Sambamba na hilo, kwa hiyo nithibitishe tu kwamba kwa kweli kama tulivyojipanga na kwa kuwa tumejitahidi kutatua changamoto zinazojitokeza na zipo bado zinaendelea lakini tunakaa vikao mara kwa mara. Tuna uhakika mpaka ifakapo Juni, 2020 tutakamilisha mzunguko wa kwanza REA Awamu ya Tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ameulizia kwenye Manispaa ya ya Morogoro, naomba nimtaarifau Mheshimiwa Mbunge mwenyewe nimeshatembelea Manispaa ya Morogoro kama mara mbili nikiwa na Mheshimiwa Aboud. Moja wapo ya maeneo ambayo tuliwasha ni maeneo ya Tungi, ni kweli maeneo ni mengi na kwa kuwa Mkoa wa Morogoro una kua sana katika ujenzi wa makazi. Maeneo haya kwa kuwa tumelitambua hilo, kama nilivyosema hapa Bungeni tuliona kwamba licha tu ya Wakala wa Nishati Vijijini kuendelea na kazi ya kusambaza umeme vijijini lakini pia tuitake TANESCO nayo ifanya kazi hiyo hiyo na kwa kuwa tumesema bei ya kuunganisha iwe 27,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kulitambua hilo katika mpango mkakati wa ndani ya TANESCO na kwa kuwa tumeona tuna umeme wa ziada unaosalia kama Megawatts 300, TANESCO kwa mwaka wa fedha 2019 itajielekeza kwanye miradi ya distribution (usambazaji wa umeme). Takribani milioni 400 zimeidhinishwa na Bunge lako Tukufu kwa ajili ya kusambaza umeme katika maeneo ambayo yanakuwa kwa kasi yakiwemo Majiji na Manispaa, ikiwemo Manispaa ya hapa Dodoma, Manispaa ya Morogoro, Jiji la Tanga, Jiji la Mwanza, Jiji la Mbeya na maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge jana nilikuwa Kondoa kukagua haya maelekezo yalivyoanza. Kweli TANESCO wameanza kazi ya kupeleka vijijini umeme na kwa kuunganisha wateja 27,000. Nimehakikisha kweli jana tu wateja zaidi ya 500 wameunganishwa baada ya maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano kwamba TANESCO sasa kazi kubwa ni kutafuta wateja na ipunguze bei ya kuunganisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilithibitishie Bunge lako tunatambua mahitaji, tumejipanga vizuri na tutaendelea kusimamia na kupambana ili lengo hili lifikie. Ahsante sana.