Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Justin Joseph Monko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Kumekuwa na changamoto za kiusalama katika Jimbo la Singida Kaskazini kutokana na jiografia yake na rasilimali zilizopo:- Je, ni lini Serikali itaongeza Vituo vya Polisi katika Kata ya Mughunga, Mgori na Merya ili kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao?

Supplementary Question 1

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, pamoja na majibu yake nina maswali mawili madogo ya nyongeza:

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ambayo tumeayaombea vituo vya Polisi yapo mbali sana na vituo ambavyo Mheshimiwa Waziri amevisema ambavyo pia ni chakavu sana. Maeneo hayo ofisi ya OCD pia ina magari matatu tu ambayo inahudumia Halmashauri ya Singida DC pamoja na Manispaa. Je, Wizara ipo tayari sasa wakati tukisubiri ujenzi wa hivyo vituo kuongeza vitendeakazi magari pamoja na mafuta ili Askari wetu waweze kufanya kazi vizuri?(Makofi)

Swali la pili; Jeshi letu la Polisi hasa Singida lina watumishi wachache mno ambao wanatakiwa kutoa huduma katika Halmashauri zetu mbili. Je, Wizara ipo tayari sasa kuongeza idadi ya watumishi hasa Askari katika Ofisi ya OCD Singida ili waweze kutoa hudama bora kwa wananchi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kweli Jimbo la Singida Kaskazini linahudumiwa na OCD wa Singida Mjini na ni dhahili kabisa kwa maana hiyo naweza hoja ya Mheshimiwa Mbunge inahitaji kufuatiliwa na kufanyiwa kazi. Kwa sababu Majimbo mawili eneo lake la kijiografia ni kubwa kwa hiyo nimhakishie Mheshimiwa Mbunge tunalichukua kwa uzito ingawa hatuwezi kumuahidi sasa hivi kwamba tutampatia gari kwa sababu gari hizo hazipo lakini pale ambao zitapatikana tutazingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo hili la kuongeza fedha kwa ajili ya huduma zingine ikiwemo mafuta, hili narudia kama ambavyo nimejibu swali ambalo limepita kwamba kadri ambavyo hali ya kibajeti itaruhusu basi bajeti ya Polisi ikiwemo huduma ya mafuta itaongezwa katika maeneo yote ni changamoto nchi nzima, ninaamini kabisa hilo Serikali tunalitambua na tumekuwa tukilifanyia kazi kwa kadri hali inavyoruhusu na ninaamini kabisa hali itakuwa nzuri zaidi siku zinavyokwenda mbele kutokana na hali ya uchumi wetu inavyokuwa vizuri.