Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 50 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 426 2019-06-21

Name

Justin Joseph Monko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:-

Kumekuwa na changamoto za kiusalama katika Jimbo la Singida Kaskazini kutokana na jiografia yake na rasilimali zilizopo:-

Je, ni lini Serikali itaongeza Vituo vya Polisi katika Kata ya Mughunga, Mgori na Merya ili kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justin Joseph Monko, Mbunge wa Singida Kaskazini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uhaba wa vituo vya Polisi nchini ikiwemo Kata za Mughunga, Mgori na Merya. Hata hivyo huduma za kiusalama kwa wananchi wa Kata hizo zinatolewa na vituo vya Polisi vya Misange na Ngimwa kwa uratibu wa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Singida Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ujenzi wa vituo vya Polisi kwa nchi nchi nzima unahitaji rasilimali fedha nyingi, Jeshi la Polisi limeweka vipaumbele vya kiusalama katika kutekeleza ujenzi wa vituo hivyo ikiwemo katika Kata ya Mughunga, Mgori na Merya na kadhalika kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo wananchi.