Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MHE. MENDRAD L. KIGOLA) aliuliza:- Miundombinu ya shule nyingi za msingi katika Jimbo la Mufindi Kusini ni chakavu:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kukarabati miundombinu ya shule hizo?

Supplementary Question 1

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize maswali ya nyongeza. Kwa kuwa Mkoa wetu wa Iringa ni mkoa ambao kwa kweli una baridi sana na wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma kwa shida kutokan ana uchakavu mkubwa uliopo wa shule zetu za msingi. Na shule zetu nyingi za msingi toka zimejengwa hazijawahi kukarabatiwa, nishukuru baadhi ya wazazi wa Mkoa wa Iringa wamekuwa wakisaidia katika ukarabati na Mheshimiwa Waziri nafikiri alikuja akaona baadhi ya shule ambazo tumeanza kuzikarabati.

Je, Serikali iko tayari sasa kusaidia angalau kidogo baadhi ya shule ule ukarabati ambao wazazi wanafanya na Serikali ikasaidia japo kidogo ili tuweze kukarabati shule nyingi za Iringa?

Mheshimiwa Spika, swali letu la pili, kwa kuwa pia sambamba na hilo, shule nyingi za sekondari maabara nyingi hazijakamilika na wanafunzi wengi sana wamekuwa wakifanya mitihani bila kusoma vizuri kwa sababu ya kutomalizika kwa maabara.

Je, Serikali sasa inasemaje kuhusiana na kumalizia maabara ambazo bado hazijaisha ili wanafunzi wetu wa Iringa waweze kusoma na kufaulu vizuri?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya dada yangu, Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mkoa wa Iringa pamoja na mikoa mingine ina changamoto hizo za uchakavu wa miundombinu. Lakini naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu safari zangu za Mkoani Iringa tulivyofika pale katika Manispaa ya Iringa alienda kunionesha akiwa na timu yake pale, miongoni mwa shule ambazo yeye mwenyewe na wadau wenzake waliweza kushiriki katika ukarabati.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, lengo la Serikali yetu ni kuhakikisha tunafanya kila liwezekanalo kufanya ukarabati wa shule hizi ndiyo maana juzijuzi Serikali yetu imetoa zaidi ya shilingi bilioni 35.5 kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunaongeza nguvukazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kubadilisha miundombinu hiyo.

Mheshimiwa Spika, lakini hata hivyo, nikiri wazi kwamba katika suala zima la maabara kweli kuna changamoo kubwa, kama lengo la Serikali lilivyo kwamba agenda yetu kwa mfano katika bajeti ya mwaka 2019/2020 ambayo nimeiwasilisha hapa Bungeni siku chache zilizopita, zaidi ya shilingi bilioni 90.08 tunazielekeza katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, lakini karibuni bilioni 58 kati ya hizo zinaenda katika elimu ya sekondari na lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba maabara tunaziimarisha katika maeneo yetu na ndiyo maana juzijuzi tumetoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 16 ambazo tunakwenda kununua vifaa vya maabara kwa vijana wanapokuwa sekondari waweze kusoma vizuri masomo yao.

Name

Ally Mohamed Keissy

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MHE. MENDRAD L. KIGOLA) aliuliza:- Miundombinu ya shule nyingi za msingi katika Jimbo la Mufindi Kusini ni chakavu:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kukarabati miundombinu ya shule hizo?

Supplementary Question 2

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, High School ya Kirando tumejenga maabara leo miaka minne, na mlileta vifaa vya maabara vinakaa chini vinaliwa na mchwa. Lini Serikali itapeleka pesa kumaliza majengo matatu ambayo yako tayari yameshapigwa bati lakini yamekaa kama vichaka vya kuchezea panya ndani?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Keissy na DC wake wa Wilaya ya Nkasi, ndugu yangu Saidi Mtanda, katika wilaya ambazo zinafanya kazi kubwa sana ya ujenzi wa miundombinu ni Wilaya ya Nkasi.

Mheshimiwa Spika, na niseme juhudi iliyofanywa na wananchi katika eneo hilo, hasa ujenzi wa hiyo maabara, juzijuzi kama nilivyosema tulipeleka fedha ili wabainishe yale maboma, nadhani hilo ni miongoni mwa maboma. Nimuagize Mkurugenzi katika vile vipaumbele ambavyo tumepeleka fedha hizi za maboma hilo liwe sehemu mojawapo, sasa sijui kama watakuwa hawajaingiza. Lakini tutafuatilia, kuhakikisha ofisi yetu maabara hiyo inakamilika, maabara iweze kufanya kazi, Mheshimiwa Keissy usiwe na hofu.