Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanzisha Wilaya ya TANESCO katika halmashauri ya Mji wa Mafinga ili kukabiliana na kasi ya ukuaji (kiviwanda na kimakazi) wa Mji wa Mafinga?

Supplementary Question 1

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alipopita pale Mafinga tuli-raise hii concern ya suala la umeme na Mheshimiwa Waziri akaahidi kutupatia transfoma tano ambazozitakwenda kwenye vijiji vya Itimbo, Isalavanu, Matanana na Ndolezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa vijiji hivyo wanasubiri hizo transfoma kwa hamu sana nimeambiwa wanashughulikia. Sasa maswali yangu mawili ya nyongeza kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi Mji wa Mafinga unakua kwa kasi kiviwanda na kimakazi kiasi kwamba uhitaji wa umeme ni mkubwa na hata TANESCO hivi sasa inakusanya mapato makubwa kushinda hata baadhi ya mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ninalouliza, je, Serikali iko tayari kujenga kituo cha kupoozea umeme ili wananchi hawa wa Mafinga ambao wanapoteza asilimia 30 ya muda wao wa kuzalisha mali, wapate umeme wa uhakika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ninaomba kuthubutu kusema kwamba, mtu aliyepewa kazi ya ku-survey maeneo ya kupeleka umeme REA Awamu ya III, hakufanya kazi yake kwa weledi na kwa ufanisi. Kwa sababu scope coverage ya maeneo mengi ya vijiji iko chini ya nusu, kiasi kwamba maeneo kama Zanzibar, Bandabichi, Dubai, Ndolezi, Rumwago, Ihongele na Matanana, ambako surveyor alisema kuna kaya 33, lakini kuna kaya 700, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba ile scope coverage katika maeneo yale REA Awamu ya III inatekelezwa, inakwenda kuongezeka? (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, ni kwamba, Mkoa wa Iringa kwa kubahatika kupitiwa na huu msongo mkuu, yaani backbone ya umeme ya umeme wa KV 400, tunatarajia kuimarisha sana ili uweze kutoa support katika maeneo mengine, hasa inapotokea kuna changamoto ya umeme. Kwa hiyo, tunategemea kwanza kuboresha kwa kuongeza hiki kituo cha umeme ambacho kitakuwa cha msongo wa 220 mpaka 33 kwa kuweka transformer mbili zenye ukubwa wa 60 MVA, kwa hiyo, mara mbili ni 120 pale Mafinga, ili uweze pia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika viwanda vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halikadhalika katika eneo la Kisada, tunategemea pale kwa ajili ya kupitiwa na hii backbone tuweke pia vituo, kituo ambacho kitakuwa ni cha msongo wa 400 KV kitakachokuwa mpaka 220 na mpaka 33 KV na kitakuwa na transformer mbili zenye saizi ya MVA 200 kila moja. Kwa misingi hiyo tunategemea kwamba eneo hilo litakuwa ni kitovu cha uimarishaji wa umeme katika nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa upande wa kusambaza umeme, ni kweli katika baadhi ya maeneo ambayo yanazunguka miji, siyo tu kwa Mkoa wa Iringa, yaani Mafinga, lakini pia hata maeneo mengine katika nchi. Tunao mradi wa kuendeleza, kusambaza umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji ambao unafadhiliwa na Benki yetu ya Afrika. Kwa hiyo, tunategemea kwamba kwa Mkoa wetu wa Iringa na maagizo haya ambayo alikuwa ameyatoa Mheshimiwa Rais utafanyiwa kazi na utakuwa mnufaika moja wapo.

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanzisha Wilaya ya TANESCO katika halmashauri ya Mji wa Mafinga ili kukabiliana na kasi ya ukuaji (kiviwanda na kimakazi) wa Mji wa Mafinga?

Supplementary Question 2

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Jimbo la Mufindi Kusini tuka kata 16, tuna vijiji 80, tuna vitongoji 365, lakini hatuna Ofisi Za TANESCO, na bahati nzuri tumeanza kujenga Hospitali kubwa sana pale Igohole na Halamshauri ya Mufindi itajengwa pale, Makao Mkuu. Je, Serikali ina mkakati gani sasa kujenga ofisi ya TANESCO kubwa kwa ajili ya kuhudumia vijiji nilivyotaja?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Umeme TANESCO limekuwa likiweka ofisi kulingana na mahitaji na uhalisia wa upatikanaji wa fedha. Kwa sasa taratibu zinazotumika ni kwamba, sehemu ambayo ina wateja zaidi ya 10,000 na laini ya umeme kutoka inapochukuliwa mpaka kufikia huko, umbali wa kilomita 500, mara nyingi imekuwa ikiwekwa ofisi. Lakini vilevile tumekuwa tukiangalia mazingira halisi ya umbali kutoka katika makao makuu ya Serikali kwa maana ya mkoa au wilaya na vilevile pale ambapo inaonekana kwamba mazingira yake ni magumu kiasi kwamba upatikanaji wa huduma ni mgumu zaidi, tumekuwa tukiweka ofisi za TANESCO na kwa kuanzia tunaweka hata zile ofisi ndogo za kuhudumia wananchi.

Kwa hiyo, niseme tu kwamba, eneo hilo litapewa umuhimu baada ya kutathmini hayo ambayo nimeyazungumza.

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanzisha Wilaya ya TANESCO katika halmashauri ya Mji wa Mafinga ili kukabiliana na kasi ya ukuaji (kiviwanda na kimakazi) wa Mji wa Mafinga?

Supplementary Question 3

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika Jimbo la Mpwapwa, ni vijiji nane tu ambavyo havijapatiwa huduma ya umeme, na Vijiji hivyo ni Kiyegea, Kazania, Tumaligo, Mkanana, Ngaramiro, Nana, Mafuto, Kiboriani, Majani na Namba 30.

Je, Mheshimiwa Waziri ni lini vijiji hivi vitapatiwa huduma ya umeme?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi katika mzunguko wa tatu, katika REA phase lll, mzunguko wa kwanza, ni kwamba tunatarajia kufikia mwezi wa sita, vijiji vilivyokuwa katika mzunguko huo viwe vimekamilika kupewa umeme na vijiji vingine vyote vinavyofuata tunatarajia kwamba vitaingia katika mzunguko wa pili ambao unategemewa kukamilika ndani ya miaka hii kufikia mwaka 2021. Kwa hiyo, vijiji hivyo kama havikuwemo katika mzunguko huo wa kwanza, basi naamini kwamba vitaingia katika huu mzunguko wa pili.