Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA (K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itawapa huduma ya umeme wananchi wa Vijiji vya Buyubi, Itwangi, Imenya, Nyambui na Mwankanga ambao muda mrefu wamekuwa watazamaji wa nguzo za umeme unaokwenda maeneo mengine?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali ilielekeza TANESCO kwamba vijiji vyote ambavyo umeme umepita juu vipatiwe umeme. Miongoni mwa vijiji 74 ambapo kuna Vijiji vya Buyungi, Imenya, Itwangi na Nyambui, je, Serikali itavipatia umeme lini katika huu msimu wa 2019/ 2020? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Naibu Waziri aliahidi wananchi wa Nyambui atawapatia umeme. Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini? Ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya swali la msingi lakini nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuuliza swali kwa wananchi wa Shinyanga kwa niaba ya Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe taarifa Kijiji cha Itwangi kimewashwa umeme tangu juzi ingawaje swali wakati linajibiwa kilikuwa hakijawashwa umeme, kwa hiyo, kimeshawashwa umeme. Kwa hiyo, wananchi wa Itwangi sasa wanapata umeme kupitia Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Buyubi pamoja na Minyami kitawashwa tarehe 17 mwezi huu wa Septemba. Kwa hiyo, wananchi wa maeneo hayo wategemee kuunganishiwa umeme katika maeneo hayo kwa wiki inayokuja. Ahsante.