Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Raphael Masunga Chegeni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI aliuliza:- Je ni nini maana ya dhana ya uchumi kukua ukioanisha na maisha ya wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri katika dhana nzima ya uchumi kukua ukioanisha na maisha ya wananchi, kinadharia kwa kweli alivyosema ni sahihi kabisa na napenda nipongeze kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekuwa ikifanya kazi sasa kurekebisha na kurahisisha maisha ya wananchi yaweze kuwa na unafuu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza; uhalisia wa maisha sasa hivi kwa wananchi ni ghali zaidi na hali ya maisha ya wananchi bado ni ngumu. Je, Serikali inaweka mkakati gani pamoja na kuonesha kwamba hata mkulima wa pamba ambaye anauza pamba yake anakopwa halipwi na bado anategemea ahudumie baadhi ya gharama zake mwenyewe, je, ni lini Serikali sasa itaachana na mtindo huu kwa kutoa guarantee kwa wakulima wa mazao yote ili waweze kuwa wanapewa bei ambazo zinawakomboa katika shughuli zao?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; sasa hivi bei ya vyakula inazidi kupanda na ukiangalia wananchi wengi wanaathirika na kupanda kwa bei ya vyakula. Gunia la mahindi sasa ni karibu Sh.100,000, je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama hizi za maisha kwa wananchi?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Chegeni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, dhana ya kupanda bei, kushuka bei ni relative. Ni Bunge hilihili mwaka jana wakati bei ya mahindi kwa mkulima ilikuwa Sh.150, ni Wabunge hawahawa walilalamika na kusema kwamba kwa nini tunafunga mipaka. Sisi kama Serikali kupunguza gharama za bei sokoni hatua tunazochukua; moja ni kupunguza gharama za uzalishaji, mbili kuruhusu soko ku-compete, competition ndiyo itakayopunguza bei ya mazao sokoni. Pale ambapo mkulima anapata hasara hakuna mtu anayekwenda kum- subsidize. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kama Serikali hatua ya kwanza hatutaingilia bei kushusha, nini tunafanya; tunayo National Food Reserve Agency na nitumie Bunge hili kuwaambia Waheshimiwa Wabunge na Wakuu wa Mikoa; pale ambapo wanaona kwamba kuna upungufu wa mazao ya chakula sokoni wawasiliane na National Food Reserve Agency ambayo ita-supply chakula katika maeneo hayo ili kupunguza presha, lakini hatutaingilia kupunguza bei ya mazao kwa sababu wakulima wa nchi hii kwa muda mrefu wamepata hasara kwa kuwafanyia control mazao yao. Huu ni msimamo wa Serikali na ieleweke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, njia ya pili, tunahamasisha Watanzania, ardhi ya Tanzania ni potential kwa kilimo, watu wafanye jitihada kuongeza uzalishaji. Supply ikiwa kubwa, demand ikiwa ndogo mazao yatashuka bei, lakini hatutafanya intervention yoyote kwenda kupunguza bei. Njia pekee tunayofanya kama Serikali ni kutumia National Food Reserve Agency kwa ajili ya ku-supply mazao ya chakula sokoni na kupitia NFRA bei itapungua, lakini kusema bei ya chakula iko juu ni relative; ni saa ngapi bei ya chakula iko chini, ni saa ngapi bei ya chakula iko juu. Kitu cha muhimu ni kufanya jitihada kama nchi kuongeza purchasing power ya watu wetu na wakulima wetu waweze kufaidika. (Makofi)

SPIKA: Lile la pamba?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE): Mheshimiwa Spika, tatizo la pamba lililojitokeza mwaka huu ni special case. Ni kama ilivyojitokeza kwenye korosho mwaka jana; Serikali ilifanya intervention. Intervention tulizozifanya mwaka jana, mwaka huu hatukuzitumia, tumeruhusu soko, minada inaendelea, wakulima wanapata pesa yao on time na competition iko wazi.

Mheshimiwa Spika, tatizo la pamba lilijitokeza katika msimu uliopita niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, halitajitokeza msimu ujao, tutaruhusu soko, hatutafanya kutangaza control ya price, Serikali itakachokifanya kwa wakulima wa pamba wasipate hasara ni ku-control gharama za input kuanzia viuatilifu, mbegu na mambo mengine, lakini siku ya mwisho sokoni tutaruhusu bei ili wafanyabiashara waende wakutane na wakulima sokoni waweze kununua bidhaa ile na mtu apate pesa yake kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, hii ilikuwa ni special case kwa sababu bei ya pamba duniani imeanguka na sababu ya kuanguka ni kwa sababu ya mtikisiko na mgogoro uliopo kati ya China na Marekani, matokeo yake pamba imekosa bei. Serikali ikaamua kutangaza bei ya Sh.1,200 na ili wafanyabiashara wasipate hasara tukaamua kufanya mazungumzo na financial institution kuwapa incentive ili waweze kwenda kununua kwa bei ya Sh.1,200.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa wakulima wa pamba mpaka kufikia siku ya Ijumaa wamelipwa bilioni 437, ambacho hakijalipwa ni bilioni 43 tu ndizo ambazo hazijalipwa na sisi tunafanya jitihada kuhakikisha by the end of this month wakulima wa pamba waweze kulipwa fedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili ili wasipate shida kwa sababu msimu unaanza tarehe 15, nitumie nafasi hii kuwaambia wasambazaji wa mbegu wote wawasambazie wakulima bila kuwauzia halafu tuta-recover gharama ya mbegu msimu utakaokuja. Sasa hivi wakulima waende shambani kwa sababu malipo yalichelewa, lakini wapo ambao hawajalipwa, kwa hiyo wapewe mbegu.

Mheshimiwa Spika, namwelewa Mheshimiwa Dkt. Chegeni, moja ya wilaya ambazo zimeathirika sana ni Wilaya ya Mheshimiwa Dkt. Chegeni, lakini tatizo hili halitajiruudia msimu ujao. Nashukuru.

Name

Khadija Nassir Ali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI aliuliza:- Je ni nini maana ya dhana ya uchumi kukua ukioanisha na maisha ya wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Urejeshwaji wa kodi kwa wakati kwa makampuni ambayo yamewekeza nchini kutasaidia kuimarisha uwekezaji nchini na hivyo kuimarisha kipato cha mtu mmoja mmoja; je, Serikali ina kauli gani juu ya hili?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu swali moja la nyongeza la mdogo wangu, Mheshimiwa Khadija Nassir, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ameuliza kuhusu urejeshwaji wa kodi, naamini ni Kodi ya Ongezeko la Thamani, kwa wanunuzi na viwanda vyetu. Kama Taifa tunatambua kwamba tulikuwa na changamoto kubwa ya udanganyifu kwenye eneo hili la urejeshwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani. Hivyo kama Serikali tulianza mkakati wa kuhakikisha tunajiridhisha na kila muamala ambao unaletwa ili kuweza kurejesha Kodi hii ya Ongezeko la Thamani kwa wazalishaji wetu, wanunuzi wetu pamoja na viwanda vyetu ambavyo viko hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi tayari tumeshalipa zaidi ya asilimia 90 ya Kodi hii ya Ongezeko la Thamani kwa watu ambao walikuwa wanatudai. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hii asilimia 10 iliyobaki Serikali tunaendelea kujiridhisha na uhakika wa miamala yenyewe na tutazirejesha kwa wakati.