Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami Barabara ya King’ori kutoka Malula Kibaoni hadi King’ori Madukani, Maruvango, Leguruki, Ngaranyuki hadi Uwiro?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara hii inapita kata nane huko kuna wananchi ambao wanafanya shughuli nyingi sana za kiuchumi lakini pia kuna taasisi hata shule iliyokuwa ya kwanza kitaifa iko eneo hilo.

Je, ni kwanini Serikali isione kwamba kuna umuhimu sasa wa kuipandisha hadhi ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami? Kwa sababu pia iko kilomita mbili kutoka mpaka wa Kilimanjaro na Arusha.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba hii barabara ina changamoto lakini Mheshimiwa Mbunge hapa anaomba kama barabara inaweza ikapandishwa hadhi, kupandishwa hadhi ni mchakato maana yake unaitoa barabara kutoka TARURA kwenda TANROAD ambayo ni Wizara nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimuombe Mheshimiwa Mbunge jambo hili inabidi lianzie kwenye halmashauri yake liende kwenye ngazi ya mkoa kwenye kikao cha halmashauri cha barabara halafu walete kwenye ngazi nyingine ya kitaifa tutaona namna ya kufanya kama inakidhi vigezo basi itapewa hadhi hiyo ili iweze kupata fedha za kutosha na iweze kutengenezwa na wananchi wa eneo hilo waweze kupata huduma kama ambavyo ndiyo matarajio Serikali.