Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janet Zebedayo Mbene

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ileje

Primary Question

MHE. JANET Z. MBENE aliuliza:- Serikali ilinunua mashine ya kujengea kutoka Marekani kwa fedha nyingi sana kwa lengo la kuitumia kujenga nyumba nyingi za watumishi, ofisi na taasisi na kadhalika kwa haraka zaidi, mashine hiyo kwa muundo wake ina uwezo wa kujenga nyumba kwa bei nafuu zaidi na hivi sasa kuna upungufu mkubwa wa nyumba za walimu, madarasa, maabara, mabweni, nyumba za wauguzi, madaktari na vituo vya afya:- (a) Je, ni nyumba ngapi na kwa gharama gani zilizojengwa na Jeshi la Ulinzi na Kujenga Taifa kwa kutumia mashine hiyo na kama zimejengwa kwa ujenzi wa kawaida zingetumia kiasi gani? (b) Je, ni kwa nini mashine hiyo haitumiki kujenga nyumba zinazohitajika wakati kuna upungufu mkubwa sana wa nyumba za Serikali? (c) Je, Serikali iko tayari kufanya tathimini na kutuletea Bungeni mpango mzima wa kuanza kutumia mashine hiyo kujenga nyumba zinazohitajika?

Supplementary Question 1

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana Serikali kwa majibu mazuri na yenye kutoa matumaini lakini pamoja na hayo nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ni dhahiri kuwa mashine hii ingetumika vizuri ingesaidia sana kuondoa upungufu mkubwa sana wa majengo mbalimbali yanayohitajika katika kila sekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kuwa Serikali imekubali kuwa sasa iko tayari kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha kuwa mashine hii inatumika vizuri zaidi. Je, ni lini sasa huo mkakati utafanywa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa upungufu wote wa nyumba za watumishi, madarasa, zahanati unafanyiwa kazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kiasi kikubwa teknolojia hii ni mpya na haijulikani vizuri, wako tayari kuitangaza ili hata private sector waitumie?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI (K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Janet Mbene, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipokee shukurani alizozitoa kwa kazi ambayo inafanyika kwa kuona kwamba kuna umuhimu wa kutumia mashine hizo. Kama nilivyojibu kwenye swali la msingi y kwamba upungufu unaokuwepo pale ni fedha za maendeleo, kama zingepatikana kazi hii ingeweza kuendelea vyema na nyumba nyingi zingejengwa kwa kutumia mfumo huo lakini kwa sababu pesa ni kidogo unakuta haiendi sambamba na mahitaji yaliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni kwamba Serikali iko tayari kwa maana ya Wizara kushirikiana na Wizara zingine kuweza kufanya kazi hiyo. Kama Wizara zingine zitakuwa zipo tayari pengine kugharamia material yale ambayo yana bei kubwa basi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa liko tayari kushiriki katika ujenzi kwa sababu ndio wenye teknolojia hiyo.