Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:- Serikali iliahidi kuanzisha Baraza la Ardhi la Wilaya ya Mbulu. Aidha, wataalam wa Serikali walifika Mbulu na kukabidhiwa majengo kwa ajili ya Baraza hilo katika Mji wa Dongobesh na Mheshimiwa Mbunge akachangia shilingi milioni tatu za kuongeza miundombinu. Je, ni lini Baraza la Ardhi la Wilaya ya Mbulu litaanzishwa?

Supplementary Question 1

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisiposhukuru kwa kweli kwa utayari wa Serikali kuanzisha Baraza la Ardhi la Wilaya ya Mbulu.

Mheshimiwa Spika, lakini bado, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri ameonesha katika majibu yake ya msingi kwamba kuna changamoto hizi za watumishi na kwa kuwa wananchi wa Mbulu bado watakuwa wanakwenda Babati ambaki ni mbali kwa kutafuta hiyo huduma. Je, ni lini sasa ataanzisha Baraza hili ili wananchi hao wasisafiri umbali mrefu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa wataalam walishakuja kuangalia maeneo ya kuanzisha Baraza hilo na tumeshawapa na jengo na kwa kuwa Wilaya ya Mbulu ni kubwa. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa kuja kuangalia na kuona eneo gani sahihi la kuanzisha barabara hilo?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza ameuliza ni lini Baraza hili litaanzishwa. Katika majibu yangu ya msingi nimesema tayari Serikali imeshatupa Wizara Wenyeviti 20 ambao watapunguza kero katika baadhi ya Mabaraza ambayo hayakuwa na Wenyeviti wa kutosha, lakini pia kuna wale ambao hawakuwa na Wenyeviti kabisa watapelekwa. Kwa hiyo, mimi nimesema kwamba tayari Wenyeviti wapo, wanachosubiri kufanya sasa ni kupata tu maelekezo ya awali (induction course) kidogo ili waweze kwenda kufanya kazi zao, wakati wowote Baraza litaanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ameuliza kwamba Baraza hilo litawekwa wapi. Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda katika eneo husika kwanza kujiridhisha na jengo lililoandaliwa, lakini pia na eneo lililopo. Kwa hiyo nitafika Mbulu ili kuweza kuona eneo sahihi ni lipi ambalo tutaweka baraza na wananchi hawatapata usumbufu.