Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bhagwanji Maganlal Meisuria

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chwaka

Primary Question

MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA aliuliza:- Kituo cha Polisi Chwaka na Kituo cha Polisi Jozani vina tatizo kubwa la gari la kufanyia doria na ulinzi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia upatikanaji wa magari mawili kwa Vituo hivyo katika bajeti ya 2018/2019?

Supplementary Question 1

MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru Waziri amejibu vizuri. Katika Mkoa nimepata gari lakini mimi nagombania Jimboni kwangu Chwaka na Jozani nipate gari kwa sababu pana vibaka, ubakaji na wananchi wameongezeka. Kama sijapata hilo gari itakuwa matatizo katika Jimbo langu.

Swali la pili, kama sijapata hilo gari hii Baniani peke yake Bungeni sitaweza kurudi kwa mara ya pili. Kwa hiyo, naomba nipatiwe hiyo gari ili niweze kurudi na wananchi wangu wapate huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache Mheshimiwa Waziri, naomba nipate gari katika Jimbo la Chwaka. Ahsante.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nimpongeze Mheshimiwa Bhagwanji kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kabisa kupigania maslahi ya askari wetu kwenye Jimbo lake. Mimi ni shahidi mara kadhaa hapa nimekuwa nikijibu maswali yake na nikiona jitihada zake na hata wananchi wake, nina hakika wanaona jitihada hizo. Kwa hiyo, kwa jitihada hizo sioni kama wananchi wake watakuwa na mashaka naye na kuacha kumrudisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na ombi lake, kama ambavyo nimejibu swali la msingi kwamba kwa sasa hivi tumepata magari machache ambayo tumeyagawa katika level ya Mikoa na gari mbili za Mkoa Kusini Unguja zimeenda kwenye Ofisi za Wilaya zote mbili. Hata hivyo, kwa kuwa gari nyingine zinakuja na kuzingatia vipaumbele ambavyo nimevieleza basi tunalichukua ombi lake na kulifanyia kazi kwa uzito unaostahili.