Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. ASHA ABDULLAH JUMA) aliuliza:- Majengo mengi ya Mahakama za Mwanzo yamechakaa sana:- (a)Je, Serikali ina mpango gani wa kuyafanyia ukarabati au kuyajenga upya? (b)Je, Serikali haioni kama Mahakama ya Mnazi Mmoja - Dar es Salaam imeelemewa na kesi nyingi hivyo iangalie namna ya kupunguza kesi?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amesema kwamba wametenga pesa kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama nyingi za Wilaya na kama alivyozitaja, lakini napenda kumuuliza, ni lini sasa Wilaya ya Temeke ambayo inatumia majengo ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke itakuwa na majengo yake?
Mheshimiwa Naibu Spika, je, kwa Wilaya mpya ya Kigamboni ambayo imeanzishwa ni lini itapatiwa Mahakama?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

Dr. Harrison George Mwakyembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Answer

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa miaka mitano wa ujenzi na ukarabati wa Mahakama zetu, Mahakama ya Tanzania ina mpango mzuri kabisa wa kujenga Mahakama ya Wilaya Temeke. Vile vile Mahakama Kigamboni Mheshimiwa Shangazi tayari imeshajengwa, tupo katika kumalizia tu na ni Mahakama ya kisasa ambayo ningeomba tu utakapomaliza Bunge hili ukaiangalie ndiyo mfano wa Mahakama ambazo tutakuwa tunajenga Tanzania kwa Mahakama zote za mwanzo.