Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. MICHAEL J. MKUNDI - (K.n.y MHE. WILFRED M. LWAKATARE) aliuliza:- Kukua kwa elimu ya uraia na ufahamu wa mambo ya kisiasa kumefanya wananchi wengi kuupokea mfumo wa vyama vingi na kuchagua wawakilishi wengi wa Vyama vya Upinzani kuongoza Kamati za Maendeleo za Kata, Halmashauri za Miji, Miji Midogo, Wilaya, Manispaa, Majiji na Majimbo ya Ubunge na Udiwani:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza kanuni, utaratibu na mfumo wa kutoa elimu na maelekezo kwa watendaji na viongozi wa Kiserikali kuyakubali na kupata ufahamu wa mabadiliko ya kisiasa yanayokua kwa kasi ili kuepusha migogoro na migongano ya usimamizi wa kazi baina ya watendaji wa Serikali na wawakilishi wa wananchi? (b) Je, kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa kuwa na uchaguzi huru na haki kama vile Tume Huru ya Uchaguzi na chombo huru cha kusimamia chaguzi za vitongoji, vijiji na mitaa?

Supplementary Question 1

MHE. MICHAEL J. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu ya Serikali bado kuna matatizo makubwa sana kwenye utendaji katika ngazi hizi za chini zinazotokana na ama na kutokuelewa wajibu wa kila upande katika kusimamia utendaji kwenye maeneo haya. Je, bado Serikali haioni sababu ya msingi kabisa kutoa elimu pamoja na majibu haya yaliyotolewa bado kuna tatizo kubwa sana kwenye usimamizi hasa nyakati za uchaguzi ambapo kumekuwa na migogoro mingi inayotokana na watendaji wanaosimamia chaguzi hizi kufanya au kutoa maamuzi kulingana na maelekezo yanayokuwa yametolewa na viongozi wa juu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kutokana na migogoro hii, Serikali haioni kwamba kuna sababu ya msingi kabisa kutokana na mapendekezo ya Katiba iliyopendekezwa kuwepo na umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ili kuondoa kabisa migogoro hii inayotokea nyakati za uchaguzi kwenye ngazi mbalimbali?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimhakikishie kwanza uzoefu wangu kwamba kati ya mwaka 1996 mpaka mwaka 2000 mwenyewe nilikuwa Ofisa Mtendaji wa Kata, kwa hiyo nina uzoefu mkubwa na kile ninachokielezea na kata yenyewe ilikuwa ni Kata ya Manzese pale Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, chaguzi za Serikali za Mitaa hufanyika kwa mujibu wa sheria na kama atatokea Msimamizi Msaidizi yeyote akatenda kinyume cha sheria, mdau yeyote anao uhuru wa kulalamika katika vyombo vinavyohusika ikiwemo kulalamika kwa Msimamizi wa Uchaguzi na hatua zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya watu ambao wanatenda kinyume cha utaratibu wa sheria ya uchaguzi ule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili, ameuliza kwamba kuna mapendekezo kwenye Katiba iliyopendekezwa. Sasa kwa sababu Katiba iliyopendekezwa bado hatua zake hazijakamilika, nashauri Bunge lako Tukufu kwamba tusiwahishe mambo, tusubiri kwanza huo mjadala wa Katiba Mpya Iliyopendekezwa ukamilike na mambo yaingizwe kwenye sheria basi hapo tutatekeleza baada ya sheria kuwa imekamilika.

Name

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. MICHAEL J. MKUNDI - (K.n.y MHE. WILFRED M. LWAKATARE) aliuliza:- Kukua kwa elimu ya uraia na ufahamu wa mambo ya kisiasa kumefanya wananchi wengi kuupokea mfumo wa vyama vingi na kuchagua wawakilishi wengi wa Vyama vya Upinzani kuongoza Kamati za Maendeleo za Kata, Halmashauri za Miji, Miji Midogo, Wilaya, Manispaa, Majiji na Majimbo ya Ubunge na Udiwani:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza kanuni, utaratibu na mfumo wa kutoa elimu na maelekezo kwa watendaji na viongozi wa Kiserikali kuyakubali na kupata ufahamu wa mabadiliko ya kisiasa yanayokua kwa kasi ili kuepusha migogoro na migongano ya usimamizi wa kazi baina ya watendaji wa Serikali na wawakilishi wa wananchi? (b) Je, kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa kuwa na uchaguzi huru na haki kama vile Tume Huru ya Uchaguzi na chombo huru cha kusimamia chaguzi za vitongoji, vijiji na mitaa?

Supplementary Question 2

MHE. ZITTO R. Z. KABWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Serikali za Mitaa ni pamoja na sheria zinazohusiana na mabadiliko ya Sheria Ndogo za Tozo na Ushuru mbalimbali. Mpaka hapo tunapozungumza, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji haikusanyi ushuru, watendaji wamegoma kwa sababu ya amri ya Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi. Mara ya mwisho nilivyouliza Waziri alisema hana taarifa na nina uhakika sasa ana taarifa. Anatuambia nini kuhusiana na kutotekelezwa kwa sheria ambayo imetungwa na Baraza la Madiwani na imepitishwa na Waziri mwenye dhamana ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hoja ambayo ameileza Bunge lako tukufu kwa sasa naielewa vizuri sana baada ya kuwa ameigusia wiki iliyopita. Niseme tu kwamba Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma ambalo linaongozwa na ACT lilipandisha ushuru kutoka Sh.15,000 mpaka Sh.50,000 kama tozo kwa wafanyabiashara na hizo ni tozo halali ambazo zinatakiwa kukusanywa na sisi tulimuagiza Mkuu wa Wilaya asimamie tozo hizo ziendelee kukusanywa kama zilivyopitishwa na Baraza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wananchi wa Kigoma wamekuwa wakilalamika na malalamiko yao mengine wameyapeleka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo, sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tumetuma timu ya watalaam kwenda Kigoma kuangalia kinachoendelea na taarifa yao hawajatuletea. Kwa hiyo, naamini wakituletea taarifa yao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe tutampa majibu sahihi zaidi.