Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka gari ya kuwahudumia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Magunguli –Mgololo?

Supplementary Question 1

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kwa kumshukuru sana Makamu wa Rais alipokuwa amekuja kwenye jimbo langu na mimi nilimwomba Ambulance siku ile na utekelezaji umefanyika nashukuru sana. Swali langu la kwanza kule jimboni kwangu nina vituo vya afya kama vitatu ambavyo viko vijijini sana hakuna magari kwa mfano pale Mninga na Mtwango ni vituo vikubwa sasa. Je, Serikali itanisaidia tena kuniletea (Ambulance katika hivyo vijiji viwili ambao wananchi wanapata shida sana?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, nina tatizo kubwa sana la watumishi wa Afya kwenye vituo vyangu vya afya na zahanati kwenye jimbo langu. Je, Wizara ya Afya ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba watumishi wa Afya tunaweza kuwapata?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kwanza kwa niaba ya Serikali naomba nipokee shukrani ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Mbunge. Katika suala lake la kwanza, anaongelea vituo vya afya vingine viwili ambavyo viko mbali sana na vina uhitaji mkubwa wa magari ya Ambulance.
Mheshimiwa Spika, naomba nimwakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni azma ya Serikali pale ambapo gari zinapatikana tutazisambaza na hasa tutazingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa sana. Sasa kama na eneo la kwake litakuwa miongoni mwa hayo maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa hakika sisi tutatekeleza hilo, lakini ni vizuri pia akatambua kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo hawakupata hata hiyo gari ambayo yeye amepata kwa hiyo kwa kadri gari zitakapopatika tutafuata uwiano unaotakiwa ili haki iweze kutendeka.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, anaongelea juu ya vituo vyake vya afya kutokuwa na watumishi wa kutosha, naomba nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge sasa hivi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tumeshatangaza nafasi 6,180,000 na naamini pale ambapo watakuwa wameajiriwa na eneo la kwake litaweza kufikiriwa kupelekewa.