Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Dalaly Peter Kafumu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:- Mwaka 2015 Serikali ilianzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga kwa lengo la kusogeza karibu huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo, lakini tangu wakati huo hadi leo hii, Mamlaka hiyo haijapatiwa fedha za kujiendesha na kutoa huduma kwa wananchi:- (a) Je, ni lini Mamlaka hiyo itatengewa bajeti ili iweze kujiendesha na kufanya kazi zake kwa ufanisi? (b) Je, ni lini Mamlaka hiyo itapatiwa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya mji huo na kujenga barabara za lami kilometa nne zilizokuwa zimeahidiwa na Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni za Uchaguzi za mwaka 2015?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naishukuru sana Serikali kwa kuendelea kujenga barabara za lami kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais. Naomba sasa nimwulize Mheshimiwa Waziri maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imekuwa ikisuasua kwa miaka minne sasa kuilea hii Mamlaka ya Miji Mdogo; na kwa kuwa Mkurugenzi mara kadhaa amesikika akisema kwamba hii Mamlaka ya Mji Mdogo inaweza kufutwa wakati wowote, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuwaita Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mtendaji wa Mamlaka hiyo ili waje hapa wapate maelekezo maalum ili waweze kuilea vizuri kama sheria inavyosema?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa idadi ya wakazi wa Mji wa Igunga sasa imezidi, wako zaidi ya 50,000 kiwango ambacho kinaruhusu kuanzishwa kwa mamlaka kamili; na kwa kuwa makusanyo ya mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pale mjini sasa hivi yanaweza kuzidi shilingi bilioni 2, kiasi ambacho kinaweza kuiendesha mamlaka kamili. Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha Mamlaka Kamili ya Mji wa Igunga?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Dkt. Dalaly Kafumu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala zima la kumwita Mkurugenzi pamoja na Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, hata kabla ya kuwaita, katika maeneo ambayo tulitakiwa kutembelea, nami mwenyewe binafsi nilitakiwa kutembelea ni pamoja na Igunga. Naomba nimhakikishie, kuna mambo mengine ambayo tutajadiliana tukiwa site, naamini naye Mheshimiwa Mbunge akiwepo, ili kwa ujumla wake tulitazame suala hili tuone namna nzuri ya kuhakikisha kwamba Halmashauri inaendelea kuwa na nguvu yake lakini na Mji Mdogo nao uendelee, kwa sababu lengo ni kuhakikisha kwamba Igunga inaendelea kwa kasi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili ambalo ameuliza kwamba kwa kiasi ambacho pesa inakusanywa na Mji wa Igunga, ifike mahali ambapo sasa iweze kujitegemea kwa kuwa na mamlaka kamili, ni jambo jema. Hata hivyo, nayo ina tafsiri yale tofauti. Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kwamba Halmashauri ya Igunga inakuwepo pamoja na vyanzo vyake kwa ujumla. Sasa kuna uwezekano mkubwa ambapo ukisema Halmashauri ya Mji ijitenge, maana yake Halmashauri nayo inategemea vyanzo kutokana na mji, ikiunganisha na vile ambavyo ni vya nje ya mji ndiyo maana Halmashauri ya Igunga inakuwepo. Kwa hiyo, ni vizuri suala hili kwa picha kubwa zaidi ili tuone namna nzuri kutoiua Halmashauri ya Igunga lakini wakati huo huo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga nayo ifanye kazi kama ilivyokusudiwa na wananchi.

Name

Dr. Mary Michael Nagu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:- Mwaka 2015 Serikali ilianzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga kwa lengo la kusogeza karibu huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo, lakini tangu wakati huo hadi leo hii, Mamlaka hiyo haijapatiwa fedha za kujiendesha na kutoa huduma kwa wananchi:- (a) Je, ni lini Mamlaka hiyo itatengewa bajeti ili iweze kujiendesha na kufanya kazi zake kwa ufanisi? (b) Je, ni lini Mamlaka hiyo itapatiwa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya mji huo na kujenga barabara za lami kilometa nne zilizokuwa zimeahidiwa na Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni za Uchaguzi za mwaka 2015?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ulivyo Mji Mdogo wa Igunga, Mji wa Katesh nao ulianzishwa kuwa Mamlaka Ndogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, lakini ni kweli kwamba Halmashauri haiipi kipaumbele hii Miji Midogo iliyoanzishwa. Je, Serikali itaweka utaratibu mzuri wa kuona hii Miji Midogo iliyoanzishwa inapata hela au kuipandisha hadhi? Kama sivyo, miji hiyo itabaki inadumaa na wakati ndiyo inayotoa mapato makubwa kwa Halmashauri. Naomba Serikali iseme wataweka utaratibu huo lini ili Miji Midogo iwe na uhakika wa kuendelea? Ahsante.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo nia ya Serikali kukiuka kile ambacho kinaitwa D by D. Kwa mujibu wa Katiba ni sisi ambao tuliamua kwamba tunapeleka madaraka kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Mbunge, kwa kupitia vikao vyetu ambavyo naye ni Diwani anaporudi kule, sisi tukiwa Madiwani kule ndiyo ambao tunafanya maamuzi kuona namna iliyo bora ya kuhakikisha kwamba Halmshauri zetu zinafanya kazi iliyokusudiwa. Itakuwa siyo busara Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenda kuziingilia zile Halmashauri ambazo Waheshimiwa Madiwani wakikaa wana maamuzi ambayo ni sahihi nasi tunakuja kubariki kutokana na vikao vyao ambavyo ni halali.