Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Uyui inajulikana kwa jina la zamani la Tabora District Council (TDC) jina ambalo linagongana na jina la Manispaa ya Tabora (Tabora Minicipality). Wilaya kupitia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa alileta maombi ya kubadili jina la Halmashauri kutoka Tabora District Council (TDC) na kuwa Halmashauri ya Uyui na Halmashauri imeomba kubadili jina la Jimbo la Tabora Kaskazini na Jimbo la uyui ikibeba jina la Wilaya na jina la eneo la kijiografia Uyui kwa sababu, hakuna tena Tabora Kaskazini, Kusini wala Magharibi:- (a) Je, ni lini jina la Halmashauri litabadilishwa kuwa Halmashauri ya Uyui? (b) Je, ni lini Jimbo la Tabora Kaskazini litaitwa Jimbo la Uyui?

Supplementary Question 1

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri ambayo yako sawasawa na matakwa ya Wanauyui, DCC pamoja na RCC. Hata hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa vile Serikali na wadau wengine wote wamekuwa wanalipa fedha zilizotakiwa kwenda Halmashauri ya Uyui, I mean Tabora District Council, zimekuwa zinalipwa halmashauri au manispaa; je, Serikali sasa itakuwa tayari kusaidia hela zote ambazo zimelipwa manispaa na manispaa wakazitumia, ili ziweze kurejeshwa katika Halmashauri ya Uyui?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa vile maelekezo ya Serikali ni kwamba, tukae sasa Baraza la Madiwani, DCC na RCC tuombe kubadilishiwa jina la Tabora Kaskazini ambalo halina Mashariki, Kusini wala Magharibi liweze kuwa Jimbo la Uyui. Je, Serikali, yeye Waziri ataunga mkono jambo hili ili liweze kupita haraka kama ambavyo tunapendekeza sisi?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, kuhusu mkanganyiko wa jina, nataka nimwambie Mheshimiwa Maige na wadau wote wa Mkoa wa Tabora na nchi nzima kwamba hakuna mkanganyiko wowote wa jina; kwa sababu Halmashauri ya Manispaa ya Tabora hailingani kwa vyovyote vile na Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, kwa hiyo, hakuna tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utendaji, wale watendaji wa Serikali wanaokosea kupeleka fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakazipeleka kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wamefanya makosa. Kwa hiyo, fedha zote ambazo zimekwenda Manispaa ya Tabora ambazo ni za Halmashauri ya Wilaya ya Tabora zinatakiwa zipelekwe Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na kama kuna fedha zilikwenda kimakosa zirejeshwe haraka iwezekanavyo.
Mheshimiwa mwenyekit, katika swali lake la pili; sisi katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kwa sababu hatuna mamlaka na jina la jimbo, tunawaunga mkono Halmashauri ya Wilaya ya Tabora ambao pengine baada ya muda mfupi ujao itakuwa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui. Wakipendekeza jina Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba, jina la Tabora Kaskazini sasa libadilishwe sisi tutawaunga mkono kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Uyui inajulikana kwa jina la zamani la Tabora District Council (TDC) jina ambalo linagongana na jina la Manispaa ya Tabora (Tabora Minicipality). Wilaya kupitia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa alileta maombi ya kubadili jina la Halmashauri kutoka Tabora District Council (TDC) na kuwa Halmashauri ya Uyui na Halmashauri imeomba kubadili jina la Jimbo la Tabora Kaskazini na Jimbo la uyui ikibeba jina la Wilaya na jina la eneo la kijiografia Uyui kwa sababu, hakuna tena Tabora Kaskazini, Kusini wala Magharibi:- (a) Je, ni lini jina la Halmashauri litabadilishwa kuwa Halmashauri ya Uyui? (b) Je, ni lini Jimbo la Tabora Kaskazini litaitwa Jimbo la Uyui?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa kuwa, Halmashauri ya Geita iligawanywa mara mbili, Geita Mjini na Geita Vijijini; na kwamba mpaka sasa Ofisi za Mkurugenzi wa Geita Vijijini ziko mjini; je, TAMISEMI inafikiriaje kumhamisha Mkurugenzi wa Geita Vijijini kurudi vijijini ambako ni Nzela ili aweze kuwa karibu na wananchi wake?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, swali hili la Mheshimiwa Musukuma ni swali la kiutendaji zaidi, naomba nilifanyie kazi baada ya kurudi ofisini.