Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joyce Bitta Sokombi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOYCE B. SOKOMBI aliuliza:- Kumekuwa na tatizo kubwa la maji katika Wilaya ya Musoma Vijijini hasa vijiji vya Kabulabula, Bugoji, Kangetutya na Saragana. Aidha, visima vilivyochimbwa na wanakijiji hao vinakauka wakati wa kiangazi. Je, ni lini Serikali itahakikisha programu za maji zinapelekwa na zinatekelezwa kwa umakini katika Wilaya ya Musoma Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mweyekiti, ahsante. Nasikitika sana kwa majibu ya Waziri ambayo yamekuwa ni hayo hayo yakijirudia. Tumeona wenzetu wa Kahama na Shinyanga wananufaika kwa kiasi kikubwa sana na mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria. Ni kwa nini Serikali imeviacha vijiji hivi ambavyo viko karibu kabisa na Ziwa Victoria kuvipatia maji muda mrefu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la usanifu limekuwa likichukua muda mrefu sana kabla miradi kuanza kutekelezwa. Je, ni lini usanifu wa mradi huu utakamilika? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu concern ya Mheshimiwa Mbunge kwa changamoto hii ya maji na ame-compare na mradi wa maji unaokuja Kahama sasa hivi unakwenda Tabora mpaka Sikonge. Ni kweli, katika nchi yetu na maeneo mbalimbali kuna changamoto ya maji lakini siyo kwamba watu wa vijiji vile wamesahaulika ndiyo maana katika jibu langu nilizungumzia mpango wa maji katika Ziwa Victoria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipofika Musoma jambo ambalo tulielekezana na wataalam ni kwamba siyo vyema watu wa mji kwa mfano ukianzia hapa Bunda mpaka unafika kule Musoma ambako ukiangalia wana utajiri mkubwa wa Ziwa Victoria halafu wakaendelea kupata shida ya maji. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Maji Awamu ya Pili ni commitment ya Serikali katika kipindi hiki cha miaka hii, tutahakikisha usanifu unakamilika lakini siyo usanifu peke yake bali mradi mkubwa huu wa maji lengo ni kuwasaidia wananchi wa eneo lile kwa sababu wakikosa maji hata huduma za uchumi zinakwama.

Name

Susan Anselm Jerome Lyimo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOYCE B. SOKOMBI aliuliza:- Kumekuwa na tatizo kubwa la maji katika Wilaya ya Musoma Vijijini hasa vijiji vya Kabulabula, Bugoji, Kangetutya na Saragana. Aidha, visima vilivyochimbwa na wanakijiji hao vinakauka wakati wa kiangazi. Je, ni lini Serikali itahakikisha programu za maji zinapelekwa na zinatekelezwa kwa umakini katika Wilaya ya Musoma Vijijini?

Supplementary Question 2

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Tatizo la maji salama na maji safi katika nchi hii ni kubwa sana na Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI na Naibu Waziri wa Maji hivi majuzi walikuwa kwenye semina maalum ya programu ya maji inayoitwa “Uko Tayari?” Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wagonjwa katika hospitali wanaugua magonjwa yanayotokana na maji machafu. Je, Serikali kupitia Wizara zote (TAMISEMI na Maji) zina mkakati gani kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama hasa katika Awamu hii ya Tano?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yake amedai kwamba kuna magonjwa mengi mahospitalini ambayo yanatokana na kutokuwepo kwa maji safi na salama. Kuanzia bajeti ya mwaka 2006/2007 tulianzisha Programu ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji ambayo ilikwenda kwa muda wa miaka mitano, imekwisha Juni, 2016 sasa hivi tumeingia programu ya pili. Malengo yetu ni kuhakikisha kwamba tunaweka fedha ya kutosha na miradi mingi sasa inatekelezwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama na kwa karibu zaidi.
Kwa hiyo, tumeshaanzisha na tumelenga kwamba itakapofika mwaka 2020 vijijini tuwe tumeshakwenda zaidi ya asilimia 85 na mijini twende asilimia 95. Kwa hiyo, tupo na tumeshaanza siyo kwamba tumekaa, tunaendelea na tutahakikisha kwamba wananchi hawapati shida ya magonjwa yanayotokana na maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini zaidi ya hapo, sasa hivi tume-centralize kuhusiana na ununuzi wa dawa za kutibu maji. Utaratibu uliokuwepo ni kila Mamlaka inanunua dawa hizo kivyake sasa tutanunua kutoka center moja kwamba Serikali sasa itakuwa inafanya bulk purchase ya dawa za kutibu maji ili tuhakikishe kwamba maeneo yote tunakuwa na maji safi na salama. (Makofi)

Name

Richard Mganga Ndassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. JOYCE B. SOKOMBI aliuliza:- Kumekuwa na tatizo kubwa la maji katika Wilaya ya Musoma Vijijini hasa vijiji vya Kabulabula, Bugoji, Kangetutya na Saragana. Aidha, visima vilivyochimbwa na wanakijiji hao vinakauka wakati wa kiangazi. Je, ni lini Serikali itahakikisha programu za maji zinapelekwa na zinatekelezwa kwa umakini katika Wilaya ya Musoma Vijijini?

Supplementary Question 3

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba niiulize Serikali, katika Wilaya ya Kwimba visima 188 vimeharibika, havifanyi kazi kutokana na kuzeeka lakini vingine vimechakaa na vimekauka.
Sasa naomba kuuliza, kwa sababu wananchi wa Kata za Mwabomba na hasa Nkalalo pale center wanashida kubwa sana ya maji kutokana na visima hivi kuharibika, je, Serikali sasa ina mpango gani wa kusaidia ili visima hivyo viweze kufanya kazi wakati tunasubiri mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hoja ya Mheshimiwa Ndassa inakwenda katika maeneo mbalimbali na tumekuwa na changamoto kubwa sana katika visima vya maji na ndiyo maana tumekuwa tukitoa maelekezo maeneo mbalimbali kwamba hivi visima vya maji recharging capacity wakati mwingine inashuka kutokana na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Ndassa kwamba katika mpango wa Serikali wa sasa hivi kuna mashindano maalum tumeyatoa kwa kila Halmashauri ya jinsi gani mipango yao mikakati watakavyozindua kuhakikisha miradi ambayo mwanzo ilikuwa haifanyi vizuri wanafanya ukarabati wa visima hivyo na kuweza kuvisimamia. Kuna mpango maalum ambao tumepata fedha kutoka World Bank ambapo zinasaidia sana katika suala zima la kuongeza nguvu za Halmashauri. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba kupitia Halmashauri zetu, ni mpango siyo wa Halmashauri ya Kwimba peke yake isipokuwa ni katika Halmashauri mbalimbali tumewaelekeza wataalam wetu wahakikishe sasa wanavikarabati visima mbalimbali viweze kutoa maji, lakini hata hivyo kuweza kusimamia vizuri kwa sababu baada ya kufanya hivyo watapata fedha nyingine zaidi kwa ajili ya kuhakikisha wanakarabati vituo vyao vya maji. Kwa hiyo, naamini Wilaya ya Kwimba itafanya hili ili wananchi wa maeneo yale waweze kuondokana na shida ya maji katika maeneo yao.