Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kasuku Samson Bilago

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. KASUKU S. BILAGO aliuliza:- Jimbo la Buyungu Wilayani Kakonko linapakana na nchi ya Burundi, hivyo raia wa nchi hizi mbili wanafanya baadhi ya shughuli za kibiashara na kijamii kwa kushirikiana kwa muda mrefu hata kabla ya Burundi kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. (a) Je, ni lini Serikali itafungua Ofisi ya Uhamiaji katika kijiji cha Muhange iliyofungwa bila sababu za msingi? (b) Je, kwa nini Warundi wakija kufanya biashara kwenye masoko ya ujirani mwema au kulima mashamba hukamatwa na kufungwa jela? (c) Je, kwa nini Warundi 254 waliofungwa kwa makosa kama hayo wasirudishwe kwao ili kupunguza msongamano magerezani?

Supplementary Question 1

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika jibu alilotoa Waziri kuhusu usalama uliosababisha kufungwa kwa Ofisi ya Uhamiaji Muhange miaka ya 1990 si la kweli. Miaka zaidi ya 20 Muhange ni salama na hakuna ofisi pale, wananchi wako pale, ofisi nyingine zote za Serikali zipo, inakuwaje Ofisi ya Uhamiaji ndiyo ishindikane kuwepo Muhange kwa sababu za kiusalama?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Burundi ni miongoni mwa Nchi za Afrika Mashariki kama zilivyo Kenya, Rwanda na kadhalika. Mipaka inayopakana na nchi hizi wananchi wake wananufaika kwa kubadilishana biashara kama mipaka ya Tunduma, Sirari, Namanga na kadhalika, pale kwetu, Jimbo la Buyungu wapo Warundi wanaokuja asubuhi kulima mashamba na kurudi nyumbani au sokoni na kurudi jioni, lakini Warundi hao wamekuwa wakikamatwa, mbona wale wa Sirari, Namanga na kadhalika hawakamatwi? Ahsante.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, nilipojibu swali langu la msingi nilieleza sababu zilizosababisha kituo kile kufungwa ni hali ya usalama Burundi, sio Tanzania. Kwa hiyo, hoja yake kwamba Muhange ni salama sio hoja ambayo nimeijibu katika swali la msingi, ni kwa sababu ya hali ya machafuko Burundi ilivyoanza, ndiyo sababu ambayo nilijibu katika swali la msingi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, ni kweli wananchi waliopo mipakani katika nchi yetu na nchi jirani, zikiwemo Burundi, Uganda, Rwanda na kadhalika, tumekuwa na mahusiano ya muda mrefu na ndiyo maana kuna utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria zetu. Kuna utaratibu ambao upo kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji wa jinsi gani raia wa kigeni wanapaswa kuingia nchini na nini wafanye na ni aina gani ya viza wawe nayo. Na tunaendelea kusisitiza kwamba sheria hizi ambazo zimetungwa kwa maslahi ya Taifa letu wananchi wa nchi jirani waendelee kuzitii.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kumekuwa kuna utaratibu wa utoaji wa vibali maalum kwa wananchi ambao wanaishi mipakani kwa masafa yasioyozidi kilometa kumi ambavyo vinaitwa vibali vya ujirani mwema. Vibali hivi vinatolewa bila ya malipo ili kuweza kuhamasisha na kusaidia wananchi ambao wamekuwa wakiishi mipakani kuendelea kutekeleza shughuli zao wanapokuwa wanavuka mipaka kwa shughuli za kawaida.

Name

Masoud Abdalla Salim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtambile

Primary Question

MHE. KASUKU S. BILAGO aliuliza:- Jimbo la Buyungu Wilayani Kakonko linapakana na nchi ya Burundi, hivyo raia wa nchi hizi mbili wanafanya baadhi ya shughuli za kibiashara na kijamii kwa kushirikiana kwa muda mrefu hata kabla ya Burundi kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. (a) Je, ni lini Serikali itafungua Ofisi ya Uhamiaji katika kijiji cha Muhange iliyofungwa bila sababu za msingi? (b) Je, kwa nini Warundi wakija kufanya biashara kwenye masoko ya ujirani mwema au kulima mashamba hukamatwa na kufungwa jela? (c) Je, kwa nini Warundi 254 waliofungwa kwa makosa kama hayo wasirudishwe kwao ili kupunguza msongamano magerezani?

Supplementary Question 2

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri, kumekuwepo na ongezeko kubwa la jamii ya Warundi katika Kambi ya Ulyankulu kule Tabora, hali ambayo inatishia usalama wa raia na mali zao, lakini zaidi wazawa maeneo ya Ulyankulu. Je, unafahamu ongezeko hili na una mikakati gani ya ziada kuweza kukabiliana na tatizo hili ili ongezeko hili lisiendelee tena?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na jitihada mbalimbali ambazo zinafanyika kuweza kuhakikisha kwamba tunapunguza idadi ya wakimbizi katika makambi yetu, na ni shahidi hivi karibuni mmeona kuna zoezi la kurudisha wakimbizi ambao wanarudi Burundi kwa hiari yao ambalo linaendelea. Hii yote ni kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Serikali yetu pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki imefanya katika kuhakikisha kwamba amani inarudi Burundi na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kawaida.
Mheshimiwa Spika, kwahiyo, kitu ambacho nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni kwamba kambi zetu zote za wakimbizi hivi tunavyozungumza, kuna pungufu la wakimbizi ambao wanaingia, lakini pia harakati za kurudisha wakimbizi Burundi zinaendelea kwa kasi kubwa sana. Niendelee kumtoa wasiwasi, lakini vilevile niendelee kuwaomba kuwa nasihi wananchi ambao wanaishi mipakani kuendelea kutoa ushirikiano wao kwa baadhi ya wale wakimbizi ambao bado wanahisi kwamba sio wakati muafaka wa kurejea Burundi kwa sasa hivi, kuendelea kuwa- host kama ambavyo tumekuwa tukifanya miaka yote mpaka pale ambapo wataamua kuondoka wote kwa pamoja.