Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hamadi Salim Maalim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Kojani

Primary Question

MHE. HAMAD SALIM MAALIM aliuliza:- Miongoni mwa stahiki za askari polisi anapohamishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ni nauli ya askari huyo na wategemezi wake pamoja na fedha za kusafirishia mizigo:- Iwapo mwajiri atashindwa kumlipa askari huyo stahiki zake zote hizo, je, askari huyo atapaswa kuhama kwa gharama zipi na kuripoti mkoa wake mpya aliopangiwa?

Supplementary Question 1

MHE. HAMAD SALIM MAALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya…
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa askari wengi hufanya kazi mbali na walikozaliwa na hulazimika kuwa pamoja na familia zao, je, askari hawa wanapohamishwa na wanachotegemea ni mshahara tu, pamoja na familia zao na mizigo yao, watahamaje kufika maeneo waliyohamishiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa kila mwaka Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani hupitishwa ikiwa na stahiki zote za askari polisi na sasa hivi askari wengi wamehamishwa, zaidi ya miaka mitatu hawajapata stahiki zao, ni lini Jeshi la Polisi litawalipa askari hao wanaodai stahiki zao za uhamisho?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kuwa na concern na maisha ya askari wetu. Hata hivyo, niseme tu kwamba askari anapohama kuna taratibu za Kijeshi pale alipokuwa anakaa ama pale ilipokuwa familia ipo huruhusiwa kukaa mpaka pale atakapokuwa amepewa fedha za kuhama na kuweza kuhamisha vifaa vyake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwepo wa madai; katika mwaka wa fedha huu uliokwisha tumetumia zaidi ya bilioni tano kulipa madeni yaliyokuwa ya askari polisi wetu na tumetumia zaidi ya bilioni saba kulipa zilizokuwa stahili za askari wetu wa Magereza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachotokea na kwa nini anaendelea kuona bado wapo wanaodai, ni kwa sababu uhitaji wa kuhama wa askari ni mkubwa kufuatana na mazingira na maeneo ambako anaweza akahitajika tofauti na watumishi wengine wa umma.