Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rhoda Edward Kunchela

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. RHODA E. KUNCHELA aliuliza:- Ipo changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana wa Mkoa wa Katavi. Na hii ni kutokana na miundombinu mibovu inayosababisha wawekezaji kushindwa kuwekeza. Je, Serikali ina mikakati gani ya kusaidia vijana hao wapate ajira na kuwa na mazingira ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi?

Supplementary Question 1

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante na nina maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, Mheshimiwa Rais kabla ya Mei Mosi alitoa kauli akiwa Hai kwamba anaondoa kero ndogo ndogo za ushuru ambazo wanalipishwa watu ambao wanafanya biashara ndogo ndogo, akina mama pamoja na vijana.
Swali langu ni kuwa kauli hii ya Rais ililenga kuondoa
kero ya huu ushuru ndogo ndogo katika Halmashauri ya Hai peke yake au katika masoko yote Tanzania nzima likiwemo Soko la Buzogwe, soko kubwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Soko la Mpanda Hoteli na masoko madogo yote yaliyoko katika Mkoa wa Katavi? Kauli hii pia inawalenga watu wa Mkoa wa Katavi?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, nilitaka kufahamu, kumekuwa na wawekezaji ambao wamekuwa wakienda kuihadaa Serikali kuomba maeneo kwa ajili ya uwekezaji, ikiwepo katika Kata ya Kekese ambako kuna mwekezaji ambaye alichukua eneo zaidi ya eka 1,000 akiwahadaa wananchi kwamba anahitaji kuwapatia ajira. Lakini mpaka sasa shamba lile analitumia kwa manufaa yake binafsi, hakuna ajira zozote alizotengeneza katika hilo shamba lililopo katika Kata ya Kekese, Manispaa ya Mpanda. Nini tamko la Serikali kumuwajibisha mwekezaji huyu kwa sababu anatumia pesa za wananchi na watu wa Katavi, vijana pamoja na akina mama wanahangaika hawaelewi nini cha kufanya?

Name

Dr. Charles John Tizeba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Answer

WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ni kweli suala la ushuru na tozo ndogo ndogo limekuwa kero ya muda mrefu kwa wakulima wa nchi hii na Rais alikwishatoa maelekezo kuanzia wakati wa kampeni na katika mikutano mbalimbali kwamba, Serikali iangalie namna ya kupunguza, kama si kuondoa kabisa shuru tozo na hizi ambazo zinashumbua wananchi na zitaondolewa sio kwahalmashauri moja moja kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba Mheshimiwa avute subira ya siku chache sana zijazo hazizidi 13 atasikia kwa kiwango gani Serikali itafutilia mbali tozo na ushuru mwingi sana ambao unasumbua wananchi mbalimbali. Tunadhamiria kufanya hivyo na tuseme tu kwamba nina hakika kila mtu atafurahi jinsi tutakavyokuwa tumeshughulikia hili tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na kwa upande wa mashamba ambayo wawekezaji mbalimbali wameyachukua kwa lengo la kuyaendeleza halafu hawayaendelezi uko utaratibu unaofanywa na Wizara yetu ya Kilimo ya Ardhi, mashamba haya yanafuatiliwa na wale wote ambao hawatekelezi masharti yale yaliyo katika mikataba yao. Mashamba haya yako katika hatua mbalimbali, mengine yameshachukuliwa yamefutwa, mengine yanaendelea kufanyiwa utaratibu wa kuyafuta ili yarejeshwe kwa wananchi au mikononi mwa Serikali.