Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Haji Hussein Mponda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA (K.n.y. MHE. ALBERT O. NTABALIBA) aliuliza:- Mwaka 2011/2012 tuliweka Mkataba kati ya Halmashauri ya Buhigwe na Hospitali ya Heri Mission, Biharu Hospitali na Mulera Dispensary juu ya kutoa huduma ya matibabu kwa wazee, watoto na akinamama bure na Serikali imetoa fedha hizo na wananchi wamenufaika na huduma hizo lakini tangu Disemba, 2015 hadi sasa fedha hazitolewi tena:- (a) Je, ni kwa nini Serikali imeacha kutoa fedha ilizokuwa ikitoa? (b) Je, ni lini sasa fedha hizo zitaanza tena kutolewa ili huduma hizo ziendelee?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Niliuliza swali kwa niaba ya Mheshimiwa Obama mimi mwenyewe naitwa Dkt. Hadji Mponda.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
La kwanza, kwa kuwa mkataba kati ya Halmashauri ya Buhigwe na ile Hospitali ya Mission umesitishwa kwa sababu ya fedha, sasa ni nini Serikali wana njia mbadala ya kutoa huduma za afya bure kwa makundi haya ya wazee na watoto?
Swali la pili, mkataba kama huo huo uliofanyika Buhigwe na mwaka 2011 - 2013 ulifanyika katika Wilaya ya Ulanga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga waliingia mkataba na Hospitali ya Lugala, ni Hospitali ya Mission, lakini mkataba ule ulidumu kwa muda wa miezi sita mpaka leo umesitishwa. Sasa swali langu ni lini Halmashauri hiyo ya Malinyi pamoja na TAMISEMI wataufufua mkataba ule kwa kurudisha huduma hizi bure kwa makundi haya mawili ya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza katika sehemu ya (a) ni kwamba nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, mkataba huu haujasitishwa, kilichotokea ni kwamba kuna fedha za quarter ya kwanza ambayo imekuja mpaka mwezi Disemba ambapo tunarajia sasa kuna pesa zingine zitakuja mpaka hivi sasa na nimesema pale mwanzo kwamba matarajio zile pesa zikishafika Halmashauri, basi lazima zielekezwe katika sehemu hizi tatu ilimradi wananchi waendelee kupata huduma.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya pili, kwa sababu hili ni suala la Hospitali ya Lugala Mission sijakuwa na taarifa nayo za kutosha, lakini nina imani kwamba mikataba yote kilichozingatiwa ni kwamba, inakwenda kutekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, uwezekano ni kwamba naomba nishauri hasa Baraza la Madiwani hasa katika vikao vyao vya Kamati ya Fedha. Lazima fedha zinapokuja, wasimamie fedha hizi maelekezo yake ni wapi, kwa sababu sehemu zingine inawezekana fedha zikapita lakini watu katika kufanya maamuzi wakaelekeza pesa sehemu ambazo siyo muafaka mwisho wake wakati mwingine mikataba inavunjika wakati kumbe kuna watu hawajatimiza majukumu yao. Imani yangu ni kwamba, kila mtu atatimiza wajibu wake ilimradi wananchi wetu waweze kupata huduma bora kwa ajili ya kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaimarika katika nchi yetu.