Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Serikali imekuwa na ahadi nyingi, nzuri za kutekeleza katika kusambaza umeme kwenye maeneo mengi ya nchi yetu. (a) Katika Wilaya ya Nyang‟hwale ni vijiji vitatu tu vya Nyang‟hwale, Nyarubele, Busegwa na Makao Makuu ya Wilaya ambavyo vina umeme; je, katika bajeti ijayo ni vijiji vingapi vya Jimbo la Nyang‟hwale vitapatiwa umeme? (b) Je, kwa nini nguzo haziletwi Kharumwa wakati wateja wengi tayari wamefanya wiring kwenye nyumba zao?

Supplementary Question 1

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri ya matumaini kwa wananchi wa jimbo la Nyang‟hwale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika kijiji cha Busorwa pameshasimikwa nguzo, nyaya zimetandazwa na transfomer zimeshafungwa takribani zaidi ya miezi minane, kwa nini umeme kijiji cha Busorwa haujawashwa?
Na kwa kuwa kuna baadhi ya vijiji kama vile Izunya, Nyashilanga, Nyamikonze, Nyijundu nguzo na nyaya za umeme zimeshatandazwa lakini transfomer hazijafungwa. Ni lini trasfomer hizo zitafungwa ili umeme huo uweze kuwashwa na kuweza kuchochea maendeleo katika vijiji hivyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Mheshimiwa Naibu Waziri nakuomba baada ya Bunge hili tuongozane pamoja mimi na wewe ukaone mradi huu unavyosuasua ili uweze kuleta changamoto ili mradi huu uweze kwenda haraka ili wananchi wa jimbo la Nyang‟hwale waweze kupata maendeleo kupitia umeme, ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa katika Jimbo la Nyang‟hwale ni vijiji vitatu tu ambavyo vimeshaunganishiwa umeme, na nitoe masahihisho kidogo, Mheshimiwa na wala siyo vijiji 61, vijiji 62 mbavyo bado kwenye jimbo lako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kijiji cha Busorwa ambacho tayari kina transformer na tayari kina nyaya zimeshafungwa kulikuwa na shida ndogo tu ya vikombe ambavyo vilikuwa havijakamilika, na hivi leo vimekamilika kesho saa tisa mchana Mheshimiwa Hussein wanakuwashia umeme pale Busorwa na mtapata umeme. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni lini vijiji alivyovitaja vitapata umeme. Ametaja vijiji vitatu lakini kuna vijiji 66 ambavyo vimepatiwa kwa nusu lakini vijiji 40 vikiwemo vijiji vya Busorwa kama ulivyotaja, Kakora, Kanegere, Nyamitongo, Nyabushishi, Nyaruzugwa, Nyaruyeye na Izuguna bado havijapatiwa umeme, kwa hiyo vyote tunavipelekea umeme kama ambavyo nimetaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuongeozana naye, kwa idhini yako kama ningepeta nafasi ningependa kwenda kushuhudia vijiji vitano ambavyo amevitaja vya Nyashilanga, Nyamikonze na Izunya ambavyo vitawashwa umeme Ijumaa ijayo. Lakini kwa ridhaa yako niombe kuongozana nawe Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili ili tukawashe umeme kwenye vijiji vyako kama ambavyo nimekusudia, ahsante sana.