Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza:- Kwa kuwa barabara kuu kwenda mikoani zina foleni na tukiangalia barabara hizo zinatumika na magari mengi ya mizigo ambayo mara nyingi huwa ni chanzo cha ajali na Watanzania wengi kupoteza maisha:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha ajali hizo zinapungua?

Supplementary Question 1

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pia namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri aliyonipatia, lakini naomba kuuliza swali langu la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imejipanga vyema kwa ujenzi wa barabara hizo. Je, Serikali ina mpango gani wa kupanua zaidi barabara hizo ili ajali zisitokee?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, upanuzi wa barabara unakwenda sambamba na bajeti. Nadhani Serikali ina mipango mizuri na imefanya kazi kubwa ya kuimarisha mitandao ya barabara nchini na sasa hivi nimesikia kuna mradi wa upanuzi wa barabara ambayo inatokea Dar es Salaam kupitia Chalinze na mbele zaidi. Kwa hiyo, ni mipango ambayo inaendelea kufanyika hatua kwa hatua kadri uwezo wa Serikali utakavyoruhusu.