Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, maombi mangapi ya usajili wa Taasisi na Madhehebu ya Dini yamewasilishwa tangu 2016 na hazijapatiwa usajili na sababu za kutosajiliwa?

Supplementary Question 1

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeangalia takwimu zilizotolewana Serikali, kati ya maombi 1,858 ni maombi 423 tu ndiyo yaliyoshughulikiwa. Maombi manne yamekataliwa, 419 yamekubaliwa. Hii ni sawa na 22.7% kwa kipindi cha miaka saba kutoka 2016 mpaka 2023. Je, Serikali haioni kwamba inachukua muda mrefu kutoa uamuzi? Ingekuwa ni vyema wakachukua muda mfupi kusema wamekubaliwa au wamekataliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, je, hamjui kwamba zipo athari zinazotokana na kuchelewa kufanya maamuzi haya?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, baadhi ya maombi yamechukua muda mrefu lakini kama nilivyoeleza katika jibu la msingi. Sababu nyingine za kuchelewesha zinatokana na waombaji wenyewe kama nilivyoeleza, kutokidhi vigezo, kutoa muda wa matazamio lakini tunataka tujiridhishe pasipo mashaka kwamba, taasisi za jumuiya tunayoisajili haiwezi kuleta athari katika jamii ya watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwepo wa athari tunatambua uwepo wake. kwa mfano, taasisi itashindwa kufungua akaunti benki, taasisi inaweza ikashindwa kumiliki ardhi na vitu kama hivyo. Kwa hiyo, tunaomba pale ambapo wanatafuta harakati za kusajiliwa wafuatae vile vigezo wanavyopewa na wataalam ili isichukue muda mrefu, nashukuru.