Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 1

MHE. SAMWELI X HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza; kwa kuwa, ahadi hii ni ya muda mrefu toka 2005 na utekelezaji wake tukienda hivi utachelewa sana na tumeleta maombi maalum Wizarani.

Je, Serikali ina kauli gani juu ya maombi maalum tuliyoleta?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Mji wa Basutu ni Makao Makuu ya Tarafa ya Basutu n ani mji ambao una wananchi wengi sana.

Je, Serikali itakuwa tayari kutenga fedha ili kujenga barabara chache za lami ndani ya mji huo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Samweli Hhayuma, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maombi maalum ambayo tayari yamefika Ofisi ya Rais, TAMISEMI na tupo kuyafanyia kazi. Kwa sababu unapoleta maombi na sisi tunatafuta fedha na tutakavyopata maana yake tutatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa swali la pili, kuhusu Mji wa Basutu, na lenyewe tumelipokea na tutaliweka katika mipango yetu. Ahsante sana.

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 2

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wetu wamekuwa wakitoa ahadi kwa wananchi kwa ajili ya matengenezo ya barabara, na Rais wetu wa Awamu ya Tano alitoa ahadi ya kutengeneza barabara Kabia ile Kata ya Ishozi kuja mpaka njia panda ya Gera ambayo inasimamiwa na TARURA, lakini mpaka leo barabara hiyo haijatengenezwa ambayo imekuwa ni maswali mengi kwa wananchi na kuona kwamba, ahadi za viongozi hazitekelezwi.

Je, ni lini sasa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami, ili sasa wananchi waweze kupita katika barabara hiyo kwa urahisi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kyombo, Mbunge wa Nkenge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, ahadi za viongozi zote zipo katika mipango yetu na kila ahadi ambayo inatolewa lazima tutafute fedha ili utekelezaji wake uwepo. Kwa hiyo, waondoe shaka wananchi, tutatekeleza ahadi hiyo. Ahsante.

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 3

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Niwashukuru sana TAMISEMI kwa kazi nzuri wanayoifanya, swali langu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara inayotoka Kata ya Burungwa – Kinamapula pamoja na Ngokolo mpaka Makao Makuu ya Halmashauri ya Ushetu pamoja na barabara ya kutoka Burungwa – Sabasabini – Ifunde inayounganisha Manispaa ya Ushetu na Manispaa ya Kahama; ni lini sasa zitafanyiwa marekebisho hizi barabara kwa sababu, mpaka sasa hazipitiki kabisa kwa wananchi wa Jimbo la Ushetu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba bahati nzuei katika eneo lake la Halmashauri ya Ushetu tumeanza utekelezaji wa barabara kwa kiwango cha lami. Na sisi tutakachokifanya tu ni kuongeza fedha kwa maana ya bajeti katika eneo lake ili barabara alizozitaja ziweze kutekelezeka. Ahsante.

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 4

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa na mimi nafasi ya kuuliza swali la nyongeza: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara nyingi za Tabora mjini zimeharibika, hasa hizi za pembezoni zikiwemo Kata za Ng’ambo, Kidongo Chekundu, pamoja na Kata za Mwinyi na nyingine. Lini Serikali itatoa fedha za ukarabati, hata kwa kukarabati kwa kutumia changarawe na moram?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu na yeye, kwamba bahati nzuri sehemu ya baadhi ya barabara ambazo ameziainisha hapa zimetengewa fedha katika bajeti yetu na zitatekelezwa katika mwaka wa fedha unaokuja. Ahsante sana.

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 5

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Na mimi naomba niulize swali dogo la nyongeza: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara iliyoko katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Kata ya Ibadakuli, inayounganisha Kijiji cha Garamba ni mbovu sana kiasi kwamba ikifika wakati wa mvua watoto wanapata tabu hata ya kwenda shule. Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba, inatengeneza barabara ile kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Kijiji cha Garamba?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Salome Makamba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, anachozungumza Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, mipango ya Serikali ni kuhakikisha barabara zote ambazo zinasumbua zinatengenezwa kwa wakati. Kwa hiyo sasahivi jukumu letu ni, moja tumetenga katika vipaumbele, lakini la pili, tunatafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji. Kwa hiyo, tutatekeleza pia barabara ambayo Mheshimiwa Mbunge ameainisha. Ahsante.

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Supplementary Question 6

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mapera kuelekea Kambarage tumeleta maombi ya dharura kutokana na mvua zilizokwisha ilitengeneza korongo kubwa sana.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Benaya Kapinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi ya Halmashauri ya Mbinga yamefika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nay apo katika hatua za mwisho za utekelezaji wa hili jambo. Ahsante.