Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 430 2022-06-22

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: -

Je, Serikali itaanza lini kutekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kilomita 10 katika Mji wa Katesh?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Samweli Xaday Hhayuma, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza utekelezaji wa ahadi hii ambapo katika bajeti ya mwaka 2021/2022 ujenzi wa kilomita moja ya barabara ya Mkapa imetengewa shilingi milioni 499.99. Ujenzi umeanza tarehe 14 Machi, 2022 unatarajia kukamilika tarehe 9 Novemba, 2022.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami kilomita moja kwa barabara za Gadafi, Joel Bendera na barabara ya Stendi. Serikali itaendelea kutekeleza ahadi hiyo ya kujenga barabara za Mji wa Katesh ili kuinua hadhi ya mji huo na maisha ya wananchi kwa ujumla kulingana na upatikanaji wa Fedha.