Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 30 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 258 2022-05-25

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:-

Je, ni lini Daraja la Mto Nduruma litakalounganisha Kata za Mlangarini, Nduruma na Bwawani Wilayani Arumeru litajengwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga Shilingi Milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la mawe katika Mto Nduruma ili kuunganisha Kata za Mlangarini, Nduruma na Bwawani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TARURA itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara hii ili kuboresha mawasiliano ya Kata za Mlangarini, Nduruma na Bwawani.