Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 57 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 748 2023-06-28

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO aliuliza: -

Je, nini hatma ya madai ya maslahi ya waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dennis Lazaro Londo, Mbunge wa Jimbo la Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, taarifa zilizopo katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinaonesha kuwa hakuna madai ya mafao ya malimbikizo ambayo yapo kwa waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero. Wafanyakazi wote waliofungua madai wamelipwa. Iwapo kuna mfanyakazi yeyote ambaye hajafungua madai, ninashauri afungue madai yake ili aweze kulipwa mafao yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za mifuko zilizopo, ahsante.