Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 48 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 633 2023-06-14

Name

Francis Leonard Mtega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbarali

Primary Question

MHE. FRANCIS L. MTEGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga minara ya simu maeneo yasiyo na mawasiliano hususan Kata za Ipwani, Miyombweni na Igava?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis Leonard Mtega, Mbunge wa Jimbo la Mbarali, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilibaini changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo mbalimbali yakiwemo Ipwani, Miyombweni na Igava ambapo Serikali imempata mtoa huduma wa kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata ya Ipwani kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidigitali. Aidha, Kata za Miyombweni na Igava zitaingizwa katika miradi itakayotekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.