Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 48 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 622 2023-06-14

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa fedha kumalizia ujenzi wa Vituo vya Afya Matwiga na Mafyeko Jimboni Lupa?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2019/2020 na 2021/2022 Serikali ilitenge kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Isangawana katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati nchini kote ikiwemo ukamilishaji wa vituo vya afya vya Matwiga na Mafyeko katika Halmashauri ya Chunya.