Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 566 2023-06-08

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Umwagiliaji wa Kata ya Ikweha uliopo Jimbo la Mufindi Kaskazini utakamilika?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Skimu ya Umwagiliaji Ikweha ni miongoni mwa skimu zilizoko katika Wilaya ya Mufindi yenye ukubwa wa hekta 500. Skimu hii ina mchango mkubwa katika kuboresha Maisha ya wananchi katika Wilaya ya Mufindi.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha za kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kupata gharama za kukamilisha ujenzi wa bwawa na miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Ikweha.